Ni baada
ya muda mrefu mpendwa wetu, Fatuma Salum kuwa katika safari huko
Mozambiki katika kutafuta maisha, ametutoka Duniani akiwa katika
maandalizi ya kurudi nyumbani kwao kuiona familia yake na Mzazi wake na
ndugu zake waishio Kinondoni maeneo ya Mkwajuni Jijini Dar es Salaam,
ambapo siku mbili nyuma ameugua ugojwa wa kuishiwa nguvu mkono na mguu
upande mmoja na kukimbizwa Hospitali na akiwa Hospitalini hapo alipata
bahati ya kuongea na mama yake Mzazi na baada ya hapo tulipata taarifa
ya kuwa amefariki akiwa katika maandalizi ambapo Ijumaa hii iliyopita
alitarajia aanze safari na Ijumaa hiyo hiyo mchana akaaga Dunia , hadi
sasa wafanya biashara wenzake kwa kushirikiana na familia ya mpendwa
wetu mwili utalala Boda na asubuhi safari itaanza, Familia ya mpendwa
wetu inatowa asante kwa wote walioshiriki kufanikisha michango yao na
kujinyima ili kufanikisha safari ya mpendwa kurudishwa nyumbani na wote
wanao endelea kutowa pesa zao na mawazo yao. shukrani ziwafikie wafanya
biasha wenzake na
Madaktari wote na ndugu na jamaa kwakufanikisha taratibu za maandalizi. (KAZI YA MUNGU)
0 comments:
Post a Comment