Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Tunaheshimu vyama vyote vya siasa nchini – Bulimba

Tunaheshimu vyama vyote vya siasa nchini – Bulimba


Na Godfriend Mbuya
Jeshi la polisi nchini limesema halipendelei chama chochote cha siasa nchini na badala yake linachofanya ni kutoa ulinzi wa kuhakikisha mali na usalama wa raia upo wakati wote.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Advera Bulimba wakati akizungumza na wananchi waliokuwa wakimuuliza maswali katika kipengele cha KIKAANGONI  kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV ambapo baadhi ya wananchi walitoa madukuduku yao kuhusu upendeleo  kwa baadhi ya vyama vya siasa nchini.
“ Jeshi la polisi halina upendeleo kwa chama chochote cha siasa nchini, ndiyo maana kila chama kikizingatia kanuni za kuomba mikutano ya hadhara kinapata ulizi kutoka jeshi la polisi, hivyo kazi yetu kubwa ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao upo hivyo tukizuia mkutano wowote ni kwea lengo la kudumisha usalama wa raia na mali zao na kupafanya Tanzania kuwa sehemu salama ya nchi.
Aidha Jeshi la polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama na taarifa watakazotoa zitachukuliwa maanani na kufanyiwa kazi mara moja, na namba za kutumika ni 111 au 112.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa