Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa
wakipata maelezo toka kwa Bi Shamsa Diwani wa kikundi cha MIVA
kinachojiusisha na uchimbaji mdogo wa madini na usio rasmi leo jijini
Dar es Salaam wakati wa mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya
madini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa
wakipata maelezo toka kwa Bi Susan Fred wa TAMICUSO ambao wanajiusisha
na uchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite jijini Arusha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa akiuliza swali
kwa Bi Martha Kayaga wa kikundi cha WAWACHISI tokea singida jinsi
wanavyochimba madini ya gypsum na kuyahifadhi katika mkutano wa wadau
wanawake katika sekta ya madini.Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.
Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa
akizungumza na wanawake wachimbaji madini wadogo wadogo(hawapo pichani)
leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere walipokutana katika mkutano kazi wa
wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa akizungumza jambo
na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi
Bi.Beng’i Issa,Bi Tertula Swai wa UN women na Kessy Edward wa Baraza la
Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
Na Daudi Manongi,MAELEZO.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito
kwa wachimba wadogo wadogo wa madini kuongezea juhudi katika uchimbaji
wa madini ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu ya uchimbaji sahihi wa
madini na kutumia teknolojia nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija
katika shughuli zao.
Profesa
Ntalikwa ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake
katika sekta ya madini wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na
mdogo uliofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
“Mimi
wito wangu kwa wachimbaji hawa ni kwamba nawaomba wajipatie elimu na
teknolojia sahihi ili waweze kujiongezea kipato katika uchimbaji
huu”,Alisema Prof Ntalikwa.
Aidha
Katibu Mkuu uyo aliwataka wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya
kuwasaidia sehemu ambazo ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala la
mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.
Pia
amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa wachimbaji hawa
wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu ya ruzuku
ikiwa na lengo ya kuwasaidia kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia
sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kwa sasa
wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji mbalimbali na wanayafanyia
kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi
Bi.Beng’i Issa amesema kuwa wao kama baraza watatengeneza programu ya
jinsi ya kupata uongozi kwa wachimbaji hao ambao utasaidia kuwakilisha
mawazo yao serikali na pia program ya kuwajengea uwezo pale ambapo
wachimbaji hawa wana mapungufu na pia kuwaunganisha na masoko kama vile
viwanda vya ndani ili visinunue malighafi kutoka nje na badala yake
wanunue hapa nchini malighafi yanatotokana na uchimbaji wa madini.
0 comments:
Post a Comment