Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi.
Mjumbe wa Bodi, Dk. Jasson Kagonza.
Mjumbe wa Bodi, Khadija Shaaban.
Mjumbe wa Bodi, Fatuma Bakari.
Mjumbe wa Bodi, Leonard Kitoka.
Mjumbe wa Bodi, Dk. Ubena John.
Katibu wa Bodi ya Shirika la Posta, Rochus Assenga.
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga, akizungumza kuhusu shirika hilo, kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Haruni Kondo, kuzungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya shirika, Dk. Haruni Kondo.
Mameneja wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya ya Shirika hilo, wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi mpya wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Meneja Mkazi Zanzibar wa shirika la Posta, Mwanaisha Saidi (katikati), Meneja wa Huduma za Barua, Fadya Zam (kulia) na Meneja Utumishi wa shirika, William Makumba (kushoto), wakiwa katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa bodi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akitoa maelezo mafupi kuhusu bodi hiyo mpya pamoja na shirika hilo kwa jumla kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), kabla waziri Mbarawa hajaizindua rasmi bodi hiyo. Kushoto Ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, akitoa hutuba yake kabla ya kumkaribisha Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa (katikati), kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakinukuu hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, akizungumza wakati alipoizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, alipokuwa akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa bodi hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa, akizungumza wakati akiizindua rasmi bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania, leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo.
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga (kushoto), akifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya shirika hilo, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa (katikati), akikata utepe mkoba wa vitendea kazi kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, (Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Mjumbe wa Bodi, Stella Nghambi, akitoa neno la shukurani baada ya Waziri Profesa Mbarawa kuizindua bodi hiyo.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa), mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
HOTUBA
YA MHESHIMIWA PROFESA MAKAME MBARAWA (MB) WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO WAKATI WA UZINDUZI WA BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA,TAREHE
20 OKTOBA, 2016, KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO, GHOROFA YA 12, POSTA HOUSE MAKAO
MAKUU.
·
Katibu
Mkuu wa Mawasiliano,
·
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania,
·
Wakurugenzi
wa Bodi,
·
Kaimu
Postamasta Mkuu,
·
Viongozi
wa Menejimenti,
·
Wageni
waalikwa,
·
Mabibi
na Mabwana,
·
PONGEZI NA SHUKRANI
Awali
ya yote napenda nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema
kwa kutujalia uhai na afya njema ya
kuweza kujumuika hapa leo na kushiriki katika uzinduzi huu wa Bodi mpya ya
Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.
Pia
nawapongeza Wajumbe wote wa Bodi na Mwenyekiti kwa kuteuliwa kuongoza Shirika
hili.
Ninawashukuru
kwa kunikaribisha ili niungane na kuzungumza nanyi wakati huu wa kuzindua Bodi
mpya. Fursa hii ni adimu kwani
imetuwezesha kufahamiana pamoja na kutafakari kwa kina juu ya changamoto
zilizopo na kuanza kubuni njia ya kuzitatua.
·
MAJUKUMU NA CHANGAMOTO ZA SHIRIKA
Mwenyekiti wa Bodi,
Leo
hii nitawakabidhi baadhi ya nyenzo na nyaraka za majukumu ya Shirika na Bodi ya
Wakurugenzi kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Bunge Na. 19 ya mwaka 1993.
Sina
haja ya kutaja majukumu haya lakini ni vyema kuanzia sasa mzingatie kuwa mawasiliano
haya kwa njia ya Posta ni kichocheo na
kielelezo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Taifa lolote duniani.
Kwa
bahati nzuri Wajumbe wa Bodi hii ni wataalamu wenye uzoefu na waliobobea katika
nyanja muhimu ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa biashara, usimamizi wa
rasilimali watu na rasiliamali fedha, sheria, TEHAMA, ubunifu katika biashara,
usalama na uendeshaji wa sekta binafsi.
·
HALI YA HUDUMA ZA POSTA KITAIFA NA
KIMATAIFA
Mwenyekiti wa Bodi,
Kwa
mujibu wa takwimu za Umoja wa Posta Duniani (UPU), mtandao wa mawasiliano kwa
njia ya Posta unajumuisha Ofisi za Posta laki sita na sitini elfu (660,000).
Huu
ni mtandao mkubwa zaidi duniani ambao pamoja na huduma nyingine una uwezo wa
kusambaza wastani wa barua zipatazo 450 bilioni na vifurushi 6 bilioni kwa
mwaka.
Hapa
Tanzania Shirika hili linaendesha mtandao wa Ofisi za Posta zipatazo 400. Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo wastani watu 120,000 katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wanahudumiwa na ofisi moja ya Posta.
Kuhusu ufikishaji barua na vifurushi katika ofisi na makazi ya watu (physical delivery of mail)
kiwango ni kidogo sana. Wastani wa 98%
ya barua zinazohudumiwa na Shirika hili hupitia katika masanduku ya barua
yalioko katika ofisi za Posta.
Kiwango
hicho kinaonyesha wazi kuwa tunalo jukumu la msingi la kupanua na kuboresha
mtandao wa huduma za Posta hapa nchini ili kufikisha huduma za kisasa za
kimtandao karibu na jamii. Ningependa
kusisitiza hapa kuwa ni lazima Shirika hili liongeze kasi zaidi katika
kuboresha na kuanzisha huduma zinazozingatia matakwa ya wateja.
·
SERA YA TAIFA YA POSTA
Mwenyekiti
na Wajumbe wa Bodi,
Kwa
hivi sasa Wizara yangu inaendelea kuhuisha Sera ya Taifa ya Posta ili
kuzingatia mahitaji ya sasa na baadae. Utekelezaji wa sera hii ni eneo mojawapo
ambalo inabidi tulizingatie.
Mwelekeo
wa sera hii kwa muhtasari ni:-
·
Kuwezesha Shirika la Posta ambalo ni
mtoa huduma kwa umma (Public Operator) kutoa na kufikisha huduma bora
kwa jamii yote na kwa gharama nafuu.
·
Kuliendesha Shirika la Posta kwa
misingi ya kibiashara.
·
Kuzifanya huduma za Posta kuwa za
kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia maridhawa ili kukidhi mahitaji mapya ya
wateja ambayo yanabadilika mara kwa
mara.
·
Kushirikisha sekta binafsi katika
kuendesha na kuwezesha shughuli za Posta ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo
na sekta nyingine kama za fedha, biashara,
afya, elimu, habari n.k
·
Wizara yangu inapenda kuona
utekelezaji wa masuala yaliyoainishwa katika sera ya Posta na kuhakikisha
uhuishwaji wa sera hii ambayo ni ya muda mrefu 2003 ili kuwezesha malengo
yanafikiwa.
·
MATUMIZI SAHIHI YA FURSA NA
RASILIMALI ZA SHIRIKA
Kwa bahati nzuri Shirika la Posta ni
moja ya Taasisi zenye rasilimali na fursa nyingi ambazo kama zikitumiwa vizuri
zinaweza kusaidia kuliendeleza Shirika.
Rasilimali na fursa hizo ni pamoja
na:-
·
Viwanja na majengo ya kuishi na ya
ofisi ambayo yako sehemu mbalimbali hapa nchini na hasa yaliyopo maeneo ya
mijini. Kwa mfano, Shirika lina viwanja
178 na kati ya hivyo viwanja 153 vimeendelezwa na 25 havijaendelezwa.
·
Mtandao mpana wa ofisi za Posta
zipatazo 400 hapa nchini ambao umeunganishwa katika ofisi za Posta zipatazo
660,000 duniani kote (Global Connectivity).
·
Uwezo mkubwa wa kutoa huduma
unganishi za kimtandao (Integration of physical and digital solutions).
·
Uwezo mkubwa wa kuboresha huduma na
biashara zilizopo na hapo hapo kuanzisha mpya .
Kwa bahati nzuri hata Sheria iliyoanzisha Shirika hili inasisitiza juu ya jambo hili.
·
Mna uwezo wa kurejesha imani kubwa ya
kihistoria (Historical Loyalty) waliyonayo wateja na wadau mbalimbali wa
Posta.
Naamini
mnafahamu kuwa mkakati huu wa kutumia
vizuri fursa na rasilimali kama hizi umefanywa na mashirika mengi ya Posta hapa
duniani na umeyawezesha mashirika hayo kuwa na mafanikio makubwa. Hali ni hivyo hivyo hapa nchini kwani, baadhi
ya mashirikia kama hili la Posta yametumia vizuri fursa na rasilimali zilizopo
na kuweza kufanikiwa.
Jambo
la msingi ni kuangalia maeneo yote hasa
sheria zenye ukiritimba zinazozuia Shirika kutumia rasilimali zake kwa ajili ya
uzalishaji mfano, sheria ya Shirika kuwa chini ya uangalizi wa Consolidated
Holding Corporation (CHC) ambapo
haliwezi kukopa au kuweka rehani vitega uchumi vyake ili kuendeleza huduma na
biashara.
·
MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI NA SIMBO ZA
POSTA
Mwenyekiti
na Wajumbe,
Anuani
za makazi na simbo za posta (Physical Address and Post code System) ni
moja ya mradi mkubwa wa kitaifa ambao mwezi Septemba mwaka huu Waziri Mkuu
Mheshimiwa Kassim Majaliwa alizindua muongozo wake mkoani Dodoma.
Aidha,
kuwepo kwa anuani zinazotambulisha makazi ya watu na rasimali za kudumu kutatoa
fursa nyingi zaidi katika utoaji na uendeshaji wa huduma za posta nchini.
Ingawa
wadau wa utekelezaji wa mfumo huu ni wengi lakini Wizara yangu na taasisi
zilizoko chini yake hususani Shirika hili la Posta, Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zina
wajibu mkubwa zaidi katika kuhakikisha manufaa ya mfumo huu yanawafikia
watumiaji wa mwisho ambao ni pamoja na wananchi wa kawaida (last mile Users). Manufaa hayo ni pamoja na:-
·
Kuwezesha huduma za usambazaji na
logistiks. Hili ni eneo linalopanuka kwa
haraka sana hapa nchini na duniani kote.
·
Kuwezesha huduma jumuishi za
kimtandao hususani za biashara (E-business), elimu (E-education),
afya (E–medicine), utawala
serikalini (E – governance) na nyinginezo.
·
Uboreshaji wa huduma za dharura na
usalama kama zima moto na uokoaji, polisi, magari ya wagonjwa, majanga kama
matetemeko, mafuriko na vimbunga.
·
Kurahisisha usajili wa huduma,
biashara, na mifumo mbalimbali kama vizazi, vifo, ndoa na talaka.
·
Kukuza utalii wa ndani na nje pamoja
na kurahisisha utambuzi wa sehemu kwa wageni.
·
Kuboresha utendaji wa taasisi
nyingine kama za Ugavi wa Nishati na Maji, Mabenki, Mamlaka za mapato, Bima na
Hifadhi ya Jamii.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa watu wote na taasisi zote
hizo zinatutegemea katika kufanikisha mfumo huu wa Anuani za Makazi na
Postikodi. Tafadhali tusiwaangushe.
7.0
HUDUMA YA POSTA MLANGONI
Mwenyekiti na Wajumbe,
Kwa kuzingatia mwelekeo huu, Shirika
hili limeanzisha huduma mpya ijulikanayo kama “POSTA MLANGONI”. Huduma hii tajwa imeanzishwa hapa Dar es
Salaam, Dodoma na Arusha.
Ni mwanzo mzuri, lakini ningependa
mwongeze jitihada katika jambo hili.
Mwelekeo wetu uwe ni kuzingatia maslahi mapana ambayo ni pamoja na:-
·
Kujenga nchi ya viwanda.
·
Kufikiwa malengo ya Dira ya Taifa ya
mwaka 2025 (Vision 2025).
·
Kupunguza umaskini na kurahisisha
utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii.
8.0 UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU
MINGINE
Mwenyekiti na Wajumbe,
Pamoja
na utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi ili kufanikisha
dhamira yetu ya kitaifa, kwa bahati nzuri nchi yetu imefikia hatua ya
kuridhisha katika kusimika miundombinu mingine muhimu ya kufanikisha dhamira
hii.
Miundombinu hii ni pamoja na:-
·
Upanuzi wa Mkongo wa Taifa na Ujenzi
wa mikongo ya mijini (Metro fiber network).
·
Ujenzi wa kituo mahiri cha kutunza
kumbukumbu (Data – Centre).
·
Uboreshaji wa mtandao wa barabara,
viwanja vya ndege na bandari.
·
Usambazaji wa huduma za nishati ya
umeme katika maeneo yote ya nchi yetu.
Nawaagiza Bodi ya Wakurugenzi,
Menejimenti, na Wafanyakazi wote wa Shirika hili changamkieni fursa za miundombinu hii.
9.0 HITIMISHO
Mwenyekiti,
Kabla
ya kumaliza hotuba yangu ningependa kusisitiza juu ya maeneo yafuatayo:-
·
Uwajibikaji, uchapakazi na
ubadilishwaji wa mtazamo (change of mind sets) ya wafanyakazi wa Shirika
hili. Tuondokane na kuendesha shughuli
zetu kwa mazoea (business as usual). Hii
ni pamoja na kuwajengea uwezo katika teknolojia ya kisasa.
·
Kuongeza udhibiti wa usalama katika
mtandao wa Shirika. Tuwe macho na
uhalifu wa kimtandao kama usafirishaji wa madawa ya kulevya, utakatishaji wa
fedha na uzingatiaji wa jumla wa sheria za nchi na Kimataifa.
·
Kuanzisha huduma ya “One Stop
Community Centre”. Hii iende
sambamba na kuimarisha huduma za uwakala kwa kutumia TEHAMA ikiwa ni pamoja na
kuwa na “Payment Switch”.
·
Eneo lingine ni kutoa huduma bora
zinazowaridhisha wateja (customer satisfaction). Hii ni pamoja na kuimarisha shughuli zenu
za masoko.
·
Kupanua wigo wa biashara, kuongeza
mapato, kupata faida na hatimaye kutoa gawiwo kwa mwenye hisa ambaye ni
serikali.
Nafahamu
baadhi ya mambo haya yako katika mipango yenu ila la muhimu ni ufuatiliaji
na utekelezaji wenu. Kwa upande wa
Serikali tunatambua na kuzingatia changamoto za msingi za Shirika hili ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa mtaji na mzigo wa kulipa pensheni za wastaafu wa Jumuiya
ya zamani ya Afrika Mashariki.
Baada
ya kuyasema hayo, sasa natamka kuwa – Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta
Tanzania, IMEZINDULIWA RASMI.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
0 comments:
Post a Comment