Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
Mamlaka
ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekanusha juu ya uvumi unaosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika eneo ka
Mkonze lililopo mkoani Dodoma.
Tamko
hilo limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa
CDA, Angela Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika
mitandao mbalimbali ya kijamii.
Bi.
Angela amesema taarifa hizo ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa
viwanja hivyo ni halali na ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo
imepewa dhamana ya ugawaji wa viwanja mkoani humo.
“Mamlaka
yetu inapenda kuutarifu Umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo
wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kuendelea kufata utaratibu kwani mamlaka hiyo ina utaratibu uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”alisema Bi. Angela.
Amefafanua
kuwa Mamlaka hiyo inapotaka kuuza viwanja hutumia utaratibu wa
kutangaza kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii pamoja na kutoa
matangazo kwa umma kwa njia ya vipaza sauti.
Aidha, Bi. Angela ametumia fursa hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kufuata taratibu za upatikanaji wa viwanja.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai Mitandaoni ya
mwaka 2015, ni kosa kwa mtu yoyote kutangaza, kuchapisha au kueneza
habari za uongo au uzushi katika mitandao.
0 comments:
Post a Comment