Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » IDADI NDOGO YA WANANCHI KUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI KUNACHANGIA KUCHAKAA HARAKA KWA FEDHA

IDADI NDOGO YA WANANCHI KUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI KUNACHANGIA KUCHAKAA HARAKA KWA FEDHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya
Huduma za Kibenki  Benki Kuu ya Tanzania


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
IDADI ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa haraka kwa fedha.
Hayo yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya Washiriki wa Warsha ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la Zanzibar, leo Machi 30, 2017 waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi zinachakaa haraka hususan shilingi 500 na shilingi 1,000/_
“Ubora wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini matumizi makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya idadi kubwa ya watu na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
Akifafanua zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni Milioni 48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio wanatumia huduma za kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya waliosalia, hutunza wenyewe fedha hizo.
Utunzaji mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia kuchakaa haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na Kibondo mkoani Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo, utakuta fedha inachakaa haraka sana, alisema Bw.Dollah.
Akielezea majukumu ya Kurugenzi ya Huduma za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria namba Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa, kusambaza na kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.
Pia Kurugenzi hii ina jukumu la kutoa huduma za kibenki kwa serikali zote mbili, (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar).
Alisema jukumu lingine kubwa la Kurugenzi hiyo ni kuhakikisha uwepo wa noti na sarafu kwa uwiano wa kutosha kwenye uchumi, “hatuwezi kuingiza fedha nyingi kwenye uchumi bila ya kuangalia uwiano wa uzalishaji na kiwango cha fedha”.aliongeza.
Akizungumzia kushuka na kupanda kwa thamani ya fedha ya Tanzania, (TZS), Mchumi Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, alisema, miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni uhitaji wa fedha yetu, (TZS), katika soko(mzunguko).
“Ili fedha yetu (TZS), iwe na thamani lazima uhitaji wake uwe mkubwa katika soko, na ikitokea kwamba fedha yetu inahitajika kwa wingi basi fedha yetu itapanda thamani na hii itatokana na kuongeza uzalishaji na kuuza bidhaa zetu nje, lakini endapo uzalishaji utapungua, na Nchi ikaingiza kwa wingi bidhaa kutoka nje, itapelekea uhitaji wa Shilingi kupungua na hivyo thamani yake pia itapungua.” Alisema Lusajo. Na kushauri taifa kama taifa liongeze thamani ya bidhaa ili ziweze kuuzwa nje na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha yetu.
Aidha, BoT, imesema, utafiti mdogo iliyofanya umeonyesha kuwa wateja wengi katika benki za biashara, wanapokwenda kuchukua fedha, hupokea fedha (noti), za thamani ya juu yaani 10,000, na 5,000 licha ya kuwa wengine wangependa kupewa fedha ndogo ndogo kwa ajili ya urahisi wa kupata chenji.

 “Ni haki ya mteja wa benki za biashara anapokwenda kuchukua fedha benki, kudai apewe fedha za chenji (fedha ndogo ndogo, yaani 500/- 1,000,000/ na 2,000/=, ili kumrahisishia anapokwenda kufanya manunuzi asipate shida ya chenji.” Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi Vicky Msina alibainisha.

Washiriki wa semina, wakiangalia noti ya Sh. 10,000, ili kutambua kama ni halali au so halali.
Maafisa wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, (kulia), na Bw. Mohammed na Mohammed Kailwa, wakijadiliana jambo kwenye komppyuta
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi.Vicky Msina, (kulia), akizungumzia kuhusu haki ya mteja wa benki ya biashara kupewa Fedha ndogondogo kama atahitaji. Kushoto ni Bw. Abdul M. Dollah. 
Bw. Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki
Bi. Flora Nkondola kutoka EFM, akitazama uhalali wa noti ya Shilingi elfu 10,000/=

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa
Baadhi ya maafisa kutoka BoT
Mtangazaji wa Channel Ten, Bi. Dorcas R. Mtenga, akizungumza






Bw. Dollah akitoa mada

Mchumi Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akitoa ufafanuazi kuhusu kwa nini thamani ya shilingi ya Tanzania inapanda na kushuka
Bw. Dollah(kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, Bw. Lwaga Mwambande
Maafisa wa BoT










0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa