Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawatangazia wananchi wote ambao Hatimiliki zao waliziwasilisha kwa ajili ya usajili, zipo tayari na sasa wafike kituo cha Huduma kwa Mteja ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Dar es salaam kuchukua Hatimiliki zao.

Orodha ya wamiliki hao inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.ardhi.go.tz na kwenye ofisi za Idara ya Ardhi za Halmashauri za Manispaa ya Temeke, Ilala, Kinondoni, Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo na Kibaha.

Mara tu uonapo jina lako katika orodha hiyo, Tafadhali fika na kitambulisho chako.
Imetolewa na:
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa