Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Frank
Mvungi-Maelezo
Watumishi wa
Umma wametakiwa kuzingatia maadili na kuacha kutumia madaraka yao vibaya kwa
maslahi binafsi hali inayoweza kuzorotesha huduma wanazotoa kwa wananchi.
Onyo hilo
limetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa
wa Kinondoni Bw. Benn Lincoln kufuatia kukamatwa kwa Afisa Afya wa Kata ya
Mbweni Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bw. Amos Ndalawa kwa makosa
ya kuomba na kupokea rushwa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU, mshtakiwa huyo alifikishwa kwenye Mahakama
ya Wilaya ya Kinondoni na kufunguliwa mashtaka mawili ya kuomba na kupokea
rushwa kinyume na kifungu namba 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mwendesha
mashitaka wa TAKUKURU Bibi. Vera Ndeoya aliieleza Mahakama kuwa mshitakiwa
akiwa mwajiriwa wa Halmashauri ya Kinondoni kama Afisa Afya wa Kata ya Mbweni
mnamo tarehe 21 Machi, 2017 alishawishi na kupokea rushwa ya shilingi laki 3 kutoka
kwa Leticia Lubala ili asimchukulie hatua za kisheria baada ya kukagua biashara
yake. Ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo
iliongeza kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 10 mwaka huu kwa vile
uchunguzi haujakamilika.
0 comments:
Post a Comment