Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » DTB YAPATA FAIDA KABLA YA KODI YA BILIONI 31 MWAKA 2016 NA MKAKATI WA KUONGEZA MATAWI

DTB YAPATA FAIDA KABLA YA KODI YA BILIONI 31 MWAKA 2016 NA MKAKATI WA KUONGEZA MATAWI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CAPTION: Mkuu wa Kitengo cha Masoko katikaka benki ya DTB, Nd. Sylvester, akiongea na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya New Afirica. Benki ya DTB Imetangaza faida kabla ya kodi ya Bilioni 30 katika mwaka wa biashara 2016.


Na Mwandishi Wetu

Diamond Trust Bank Tanzania Limited (DTB) kwa mara nyingine imetangaza mafanikio katika taarifa ya kifedha ya mwaka 2016. Faida kabla ya kodi kwa mwaka 2016 imeongezeka kutoka shilingi bilioni 27.3 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 31.0 kwa 2016.

Amana za wateja za DTB zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 737 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 800 mwaka 2016. Jumla ya rasilimali za benki ni shilingi bilioni 984 mwaka 2016 ukilinganisha na shilingi bilioni 900 kwa mwaka 2015.

Mikopo kwa wateja imeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 565 mwaka 2016 toka shilingi bilioni 536 kwa mwaka 2015. DTB Tanzania vile imeendelea kuthibiti mikopo isiyolipika na kubaki chini ya 3% ukilinganisha na 9.5% ya sekta ya benki.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko katikaka benki ya DTB, Nd. Sylvester, akiongea na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya New Afirica. Benki ya DTB Imetangaza faida kabla ya kodi ya Bilioni 30 katika mwaka wa biashara 2016.katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Nd. Viju Cherian na kushoto ni mkuu wa kitengo cha Fedha, Nd. Joseph Mabusi

Akiongea na wanahabari Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Ndugu Viju Cherian alisema kwamba, “Ongezeko la faida kwa DTB Tanzania, hasa kwa mwaka 2016 ambapo benki nyingi zimekua kwa kiwango kidogo ni ushuhuda tosha wa muundo wa DTB Tanzania wa kihafidhina ulio na ufanisi wa hali ya juu. “Alisema pia “Utekelezaji wa mpango mkakati wao wa mwaka 2008 ulioifanikisha DTB Tanzania kufungua matawi 20 ndani ya miaka minane ni jambo ambalo limechangia katika kukuza amana za wateja na kutuwezehsa kutoa mikopo kwa riba nafuu zaidi.


Huduma bora kwa wateja,mtandao wa matawi pamoja na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya kila aina ya mteja ni sifa zilizopelekea ukuaji wa DTB Tanzania kwa mwaka 2016. “DTB Tanzania haina mpinzani katika kutoa huduma bora na kutekeleza mahitaji ya mteja. Tunaendelea kuwa wabunifu na kuwekeza kwenye teknolojia kama njia ambayo itatuwezesha kuwa karibu zaidi yateja wetu.” Aliongeza Ndugu Cherian.

Mwaka 2016 DTB Tanzania ilifunfua matawi mawili jijini Dar es Salaam na kifuikisha matawi 11 jijini Dar es Salaam na jumla ya matawi 26 nchi nzima. Tawi la CBD (Central Business District) kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Mirambo katika jengo la Diamond Plaza lilifunguliwa Machi 2016 na Tawi la Mbezi Chini lililoko Mbezi Beach katika kata ya Kawe lilifunguliwa Octoba 2016. Malengo ya DTB Tanzania kwa mwaka 2017 ni kufungua matawi yasio pungua manne ifikapo Disemba. Matawi ambayo yako kwenye mpango wa kufunguliwa hivi karibuni ni pamoja na Tawi la Uhuru, Kariakoo na Tawi la Mlimani City, Mwenge.

Katika kutambua ukubwa wa Tanzania kijiografia na haja ya kutaka kufikia wateja wengi zaidi DTB Tanzania imeanza mchakato wa kuwekeza katika mradi wa kuanzisha huduma ya kupitia mawakala. Huduma hii itaongeza wigo wa DTB Tanzania si mjini tu bali hata vijijini ambako benki nyingi hazijaweza kufika huku ikiwasogeza Watanzania huduma za kifedha karibu zaidi.Huduma hii inatarajiwa kuanza ndani ya nusu ya pili yam waka 2017.

DTB Tanzania pia imeendelea kupiga hatua kiteknolojia kwa kuboresha mfumo wake wa kibenki na kuja na mfumo wa Flex Cube V12.0 ambao una uwezo wa kiutendaji zaidi kutokana na mahitaji. Huduma ya DTB Mobile Banking ijulikanayo kama Touch 24/7 pia imeboreshwa na sasa mteja anaweza kufanya miamala ya kibenki popote alipo. iBank ambayo ni huduma ya benki hiyo kupitia mtandao wa intanetia pia imeboreshwa katika hali ya kumridhisha mteja zaidi.

Mtandao wa matawi ya DTB Tanzania ni kama ifuatavyo, Dar es Salaam: (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, barabara ya Nelson Mandela karibu na makutano ya Tabata, Upanga barabara ya Umoja Wa Mataifa, CBD kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Mirambo na Mbezi Chini Kawe. Matawi mengine ni pamoja na Arusha (2), Mwanza (2) na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na Zanzibar.

DTB Tanzania ni sehemu ya DTB Group, ikiwa na matawi zaidi ya 130 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni mshirika wa Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED), mkono wa maendeleo ya kiuchumi wa Mfuko wa Kimaendeleo wa Aga Khan. On Wednesday, March 29, 2017 4:21 PM, khalfan said wrote: Habari za mchana kuta wadau, pokeeni codes

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WANANCHI binafsi wanaweza kwenda kwenye mabenki na kuomba mikopo ya fedha za ujenzi, (Mortgage Finance), bila ya kuanza kupitia kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi-Usimamizi wa Mabenki  Benki Kuu ya Tanzania, (BoT),  Bw. Eliamringi Mandari, (pichani juu), wakati akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa mikopo ya fedha kwa ajili ya ujenzi, (Mortgage Finance) na utunzaji taarifa mteja (mkopaji) katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank) kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha leo Machi 29, 2017 inayoendelea kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (tawi la Zanzibar), mjini Unguja.
“Watu wengi hawajui kama kuna fursa hii ya ku-mortgage, kwa maana ya kujenga, kununua au kurekebisha nyumba yako, na katika kudhamiria kufanya hayo, benki inaweza kutoa masharti ambayo ni ya kurejesha fedha (mkopo) huo kwa muda mrefu kati ya miaka 5 hadi 20.” Alisema.
Hata hivyo alisema kama ilivyo kwa masharti mengine yahusuyo kukopa, hata fursa hii ya kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi vigezo na masharti pia huzingatiwa ili benki iweze kutoa mkopo huo.
Aidha kuhusu mfumo wa taarifa unaosaidia mkopeshaji,(lender), kumjua mkopaji, (borrower), ujulikanao kama, Credit Reference System, (DBS), alisema Sheria namba 48 ya BoT kuhusu masuala ya kubadilishana taarifa za mikopo, kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha inalazimisha mabenki na taasisi hizo kutuma taarifa za wateja (wakopaji), kwenye Databank ya BoT kila mwezi, alisema Bw. Mandari
Alisema pia BoT, inaandaa utaratibu utakaolazimisha wakopeshaji binafsi na Taasisi za Kibinafsi, (NGOs), zinazojihusisha na utoaji mikopo, kusimamiwa, (Regulated), katika utoaji wa taarifa za mteja (mkopaji), katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank), ili kuwaondolea usumbufu wananchi.
 “Ni kweli Sheria  inaitaka Benki Kuu kusimamia taasisi za fedha zinazochukua amana kutoka kwa wananchi, kwa kuwasilisha taarifa hizo za wakopaji kwenye mfumo huo wa BoT wa Databank, lakini kwa sasa wakopaji binafsi na taasisi za hiari zinazojishughulisha na utoaji mikopo ya kifedha, bado sera inaandaliwa ili na wao waweze kusimamiwa.” Alisema.
Alisema, wakopaji binafsi na NGOs zinazojihusisha na utoaji mikopo, zimekuwa zikitumia mabavu wakati mwingine katika kufuatilia marejesho ya mikopo kutokana na utaratibu usio wazi wa kukopa, na wakati mwingine wakopaji wanarejesha mikopo kwa riba kubwa, alifafanua.
 Bw. Eliamringi Mandari, akiwasilisha mada hiyo
Meneja Msaidizi Msoko ya Ndani wa BoT, Bw.Genes Kimaro,  akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa Sera ya Fedha wa BoT.
 Bw.Genes Kimaro
 Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa BoT, Bw.Mohammed Kailwa, (kushoto), akijibu baadhi ya hoja wakati akisaidiana na Meneja wa Masoko ya Ndani, Kurugenzi ya Masoko ya Fedha (BoT), Bw.Reverian Felix
 Baadhi ya waandishi wa nhabari za Uchumi na Fedha wanaohudhuiria semina hiyo
Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw. Richard Malisa, akitoa mada jinsi Bodi ya Bima ya Amana inavyokinga amana za wananchi

 Mwandihi wa Clouds TV, Bw. Austin Beyadi, (kulia), akihariri habari wakati semina ikiendelea. Kushoto ni Grace Semfuko wa Star Tv.
 Mmiliki wa Mtandao wa TZ Business News Online, Jaston Binala, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT Bw. Lwaga Mwambande, (kulia), akifafanua jambo wakati wa semina hiyo
 Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina, (kushoto), akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari Zanzibar, (ZBC), wakati wa mapumziko ya mchana ya semina hiyo.
Mwenyekiti wa Semina, ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Bw. Ezekiel Kamwaga, akizungumza kwenye semina hiyo
 Bi. Vicky Msina, (kulia), na Bw. Lwaga Mwmbande kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, wakifuatilia mijadala na mada zilziokuwa zikitolewa
 Bi. Vicky (kulIa), akiwa na Bi. Flora Mkemwa kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT
 Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akifuatilia mjadala






























0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa