Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » GLOBAL PEACE FOUNDATION(GPF) TANZANIA WASHIRIKI KONGAMANO LA MWANAMKE NA UONGOZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

GLOBAL PEACE FOUNDATION(GPF) TANZANIA WASHIRIKI KONGAMANO LA MWANAMKE NA UONGOZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano hilo la Mwanamke na uongozi wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Martha Nghambi ambaye (hayupo pichani)
 Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika kongamano hilo lililo andaliwa na Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam(DARUSO) Bi. Shamira Mshangama Mh. Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wote waliohudhuria katika kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na Kumkaribisha Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo
Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano hilo
Meneja wa Benki ya NMB PLC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salalaam Bi. Rehema Mwibura akielezea safari yake ya uongozi mpaka hapa alipofikia sasa na kuwaatha vijana wakike wasikate tamaa kwa kuwa wanaweza.
 Mwanachama wa zamani wa USRC Bi. Yunge Kanuda akiwasihi vijana wanawake kuwa wanayo nafasi ya kugombea ngazi mbalimbali za uongozi hivyo wanatakiwa wathubutu ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali inayoendelea 
 Mkurugenzi Mkazi wa GPF Bi Martha Nghambi(Kulia) akifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano hilo

Aliyekuwa Spika wa Bunge la USRC kwa mwaka 2014/2015 Protus Petro akielezea juu ya uongozi 
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Irene Ishengoma na aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus 2016 akielezea mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake na kuwasihi kuto bweteka kwa kuwa wanaweza.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiuliza maswali na kuchangia mawazo katika Kongamano hilo.
 Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Consolata Chikoti akifuatilia kwa makini mijadala ikiendelea.
Washiriki katika Kongamano hilo
Picha zote na Fredy Njeje



Na Dickson Mulashani

Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Tanzania na wadau wengine aliandaa kongamano kwa ajili ya Mwanamke na Uongozi likiwa na lengo la kuwafanya wanawake wapate kutambua kuwa wanaweza kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali bila kuwa na uoga wowote



Akizungumza katika Kongamano hilo Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa " GPF ni ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla."





Pia Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndio mfano kwao "Role Model" watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya chini mpaka uongozi wa juu.

 



Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika Kongamano hilo aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yake katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali bila wasiwasi.

 

Mh. Sophia Mjema aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke tamaa hizo.



Aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa wao wanaona mambo mengi zaidi katika jamii 



Mwisho alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneo la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu, alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi zaidi.    






0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa