Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Tigo: Wateja wafurahia huduma za kibiashara za uhakika

Tigo: Wateja wafurahia huduma za kibiashara za uhakika

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mwandishi Wetu


Katika hali ya kukabaliana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja, Tigo imeendelea kubuni bidhaa na huduma kwa wateja wenye biashara zinazosadifu sehemu tofauti ndani ya soko la Tanzania.



Huduma hizo za Tigo kwa ajili ya makampuni na biashara mbalimbali zinajumuisha aina tofauti za huduma za mawasiliano kwa simu (voice), SMS, pamoja na vifurushi vya data.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii  hivi karibuni jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Hussein Sayed alisema kuwa  huduma hizi ni kwa ajili ya wamiliki wa makampuni na biashara  ambao wako makini kuhusu  suala la gharama. Vile vile huduma hii inatoa viwango vya ushindani   hadi kufikia asilimia 70 ya viwango vilivyopo katika soko.

“Licha ya kufurahia viwango bora zaidi katika soko na  usimamizi wa hali ya juu wa akaunti, wateja wanawezeshwa kukamilisha biashara zao kwa kutumia mtandao mkubwa na wenye kasi ya intaneti ya 4G LTE ulioenea katika miji 22 ya Tanzania wakati huo huo wakifurahia  vifurushi vya data vya Tigo,” alisema Sayed na kuongeza kuwa  wateja watapata  kifurushi mara mbili kila wanaponunua kifurushi cha data  cha zaidi ya shilingi 25,000 ambayo  ni  promosheni tuliyo nayo kwa muda sasa.

“Kama nyongeza wateja wapya watakuwa wanafurahia kupata data za bure  ikiwa ni ofa iliyozinduliwa na Tigo katika kuwaunga mkono wafanya biashara wa Tanzania  katika uendeshaji wa shughuli zao za kila siku,” alisema Sayed.

Akizungumzia  huduma za kampuni hiyo ya simu; Sayed alisema kuwa zimeundwa kwa umakini  hivyo kwamba  huduma zote zitawapatia wateja  thamani zaidi na wakati huo huo zikiwasaidia  kupunguza gharama za mawasiliano.

Aliongeza, “Kuunganishwa na mawasiliano ni jambo muhimu katika kufanikisha miamala ya kibiashara kwa karne hii ya  21; na ndio maana  tupo makini katika kubuni huduma/bidhaa mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya biashara kubwa,za kati na ndogondogo katika soko la Tanzania.”

Sayed alisema kuwa  mafanikio ya Tigo katika utoaji wa huduma zinazolenga  biashara nchini kumechangiwa na kampuni kufanya uwekezaji mkubwa katika vifaa ndani ya kituo cha kutunza kumbukumbu (Data centre), teknolojia za huduma kwa intaneti na kuwapa mafunzo ya uhakika wafanyakazi na kuwajengea uwezo ambao wamekuwa wakiwapatia wateja suluhisho zuri katika mahitaji yao ya kibiashara.

Mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa