Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ISRAEL, EHUD BARAK AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII, APOKELEWA KIA NA WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ISRAEL, EHUD BARAK AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII, APOKELEWA KIA NA WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na familia ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii nchini. Waziri Mkuu huyo wa 10 wa Israel aliliongoza taifa hilo mwaka 1999 - 2001.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (wa pili kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe muda mfupi baada ya kuwasili na ndege ya shirika na ndege la Israel (Israel Air) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimuongoza mgeni wake, Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (kushoto kwake) kuelekea kwenye maandalizi ya ziara yake ya kitalii nchini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa