Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema Kampuni
ya madini ya Acacia imekubali kufanya mazungumzo na Serikali ikiwa ni
pamoja na kulipa fedha ambazo Serikali inaidai kwa kufanya shughuli zake
hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation
inayomiliki kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton leo
Ikulu jijini Dar es Salaama, Rais Magufuli amesema kampuni ya Barrick
imekubali mazungumzo na Serikali ya Tanzania na kulipa fedha
wanazodaiwa.
“Serikali
inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya
majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia
makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo
itakavyoendesha shughuli zake nchini kwa maslahi ya pande zote mbili”
alisema Rais Magufuli
Rais
Magufuli alisema kuwa licha ya kampuni hiyo kukubali kulipa fedha
wanazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania
kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu hapa nchini.
Nae,
Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya
mazungumzo na Serikali ya Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande
zote mbili ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo inatakiwa kulipa
kwa Serikali ya Tanzania.
Mazungumzo
hayo kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kampuni ya Acacia
yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Ian Myles na Waziri wa Katiba
na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
0 comments:
Post a Comment