NA MAGRETH KINABO – MAHAKAMA YA TANZANIA
Mahakama ya Tanzania, kupitia Mpango Mkakati wake wa Miaka Mitano 2015/16 hadi 2020 inatarajia kujenga Kituo cha Pamoja ikiwa ni hatua ya kupanua wigo wa huduma watu wenye mahitaji maalum.
sKupitia mpango Mahakama ya Tanzania inanzisha kituo hicho ikiwa hatua ya kuwapunguzia wananchi gharama za fedha wanazozitumia na muda wanaoutumia sambamba na utoaji wa haki kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji Kituo Maalum cha kushughulikia masuala ya mirathi, ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam.
“Tuna mpango wa kuanzisha kituo hicho cha huduma za Mahakama kuhusiana na masuala ya mirathi, ambacho kitakuwa na wadau mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania ili kuhakikisha huduma za mirathi zinatolewa kwa wakati bila kupoteza muda na gharama,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha kituo hicho pia kitawasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zilizo kaa muda mrefu Mahakamani,ikiwa ni moja ya mkakati wa Mahakama wa kupitia mpango huo.
“Katika Mpango huo Mahakama inatarajia kujenga Kituo Kimoja cha Pamoja kitakachoshughulikia masuala ya mirathi, hivyo huduma hizo zitakuwa zinapatikana kwenye jengo moja ili kuweza kuwaondolea usumbufu watu wanaohitaji huduma za Mahakama,” alisema Mhe. Mugeta.
Mhe . Mugeta alisema kituo hicho, kitakuwa na huduma za Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya na Mahakama Kuu. Pia kitasaidia watu wanaohitaji huduma hiyo kupatiwa haki zao kwa wakati na kuwazesha kuendelea kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kuchangia kuinua pato la Taifa.
Kituo hicho cha pamoja, kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2019 katika jiji la Dar es Salaam katika wilaya ya Temeke karibu na kituo cha polisi Chango’mbe kwenye eneo ilipo, Mahakama ya Mwanzo Temeke.
Mhe. Mugeta aliongeza kwamba kituo hicho, kinajengwa katika jiji hilo, kwa sababu asilimia 10 ya Watanzania wanaishi kwenye eneo hilo.
Alifafanua kwamba kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na vyanzo vya habari mbalimbali mirathi na mambo ya kifamilia, ni maeneo yamekuwa na changamoto nyingi.
Hali inayosababisha kuhitaji mtazamo wa pekee ili kuongeza ufanisi na tija katika kushughulikia kesi zinazohusiana na masuala ya mirathi na mambo kifamilia.
Mahakama ya Tanzania iliandaa Mkutano Maalum wa Mashauriano na Wadau wa Mahakama ili kuweza kujadiliana na kubadilisha uzoefu katika changamoto zinazojitokeza kila wakati kwenye kesi zinazohusiana na maeneo hayo.
Akizungumzia kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika kesi hizo, Mhe. Mugeta alisema upatikanaji wa haki kwa wakati mwingine unakuwa ni mgumu kwa sababu baadhi ya ndugu au familia kutowasilisha vilelezo Mahakamani kwa wakati.
Aidha Mhe. Mugeta ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema kituo hicho, kitaanzishwa katika jiji hilo kwa sababu hilo, limeonekana kuwa ni kubwa kwa sababu lina wakazi wengi.
Aliitaja sababu ya kuanzishwa kituo hicho, kimetokana kwamba Mahakama ya Tanzania huwa inapokea maoni 3,000 kila siku kuhusiana na masuala hayo.
“Kituo hicho kitakuwa na huduma za Mahakama za Mwanzo, Wilaya na Mahakama Kuu, ili kuweza kuondoa vipingamizi katika utoaji wa huduma hizo.
Mhe. Mugeta alisema katika kituo hicho, kinatarajiwa kuwa na huduma za kibenki pamoja na huduma za mafao kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii, huduma za msaada wa kisheria, usajili wa vizazi na vifo na huduma nyinginezo.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo, walipendekeza kwamba elimu zaidi itolewe kuhusiana na masuala ya mirathi.
Miongoni mwa wadau walioshirikishwa katika mpango huo ni umewashirikisha baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania, wakiwemo wadau hao, ambao ni Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWJA), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni Mafao kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS) na Baraza Kuu la Waislaamu Tanzania(BAKWATA).
IFUATAYO NI CAPTION YA PICHA YA PAMOJA
Baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania na Wadau wa Mahakama wakiwa katika Picha ya Pamoja.
0 comments:
Post a Comment