Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Serikali inatarajia kutoa
huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa kielekroniki katika
kivuko cha Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Akiongea
na Maelezo Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme Dkt. Musa Mgwatu alisema kukamilika kwa mfumo huo utakaogharimu
bilioni 1.1 kutasaidia kuiongezea mapato serikali kwani mfumo huo
utafanyakazi kwa njia za kielekroniki.
“Ujenzi
wa mashine za kielektroniki umeshaanza na kukamilika kwa upande wa
magogoni, Mkandarasi anatarajia kuanza ufungaji wa mashine hizo upande
wa Kigamboni wiki hii,” alifafanua Dkt. Mgwatu.
Dkt.
Mgwatu alisema Mkandarasi wa mradi huo anatarajia kukamilisha uwekaji
wa mashine hizo julai 25 mwaka huu na utumiaji wa mashine hizo utaanza
kutumika tu mara baada ya makabidhiano kutoka kwa mkandarasi.
Akizungumzia
gharama za kuvuka Dkt. Mgwatu amesema, gharama za kuvuka zitabaki pale
pale na hakutakuwa na ongezeko lolote mashine hizo zitakapoanza
kutumika.
Bwana
Ismail Juma, mkazi wa Kigamboni amesema kuanzishwa kwa mfumo huo
kumekuja wakati muafaka na kutasaidia kuiongezea mapato serikali na
kuepusha upotevu wa mapato katika vivuko hivyo.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano aliwaagiza
TEMESA kufunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao
utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment