Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WFT, TGNP MTANDAO,HAWA NA OXFAM TANZANIA WAWAKUTANISHA WANAWAKE VIONGOZI KATIKA KUJADILI MASWALA YA KUMKOMBOA MWANAMKE KISIASA NA KIUCHUMI, SERENA JIJINI DAR.

WFT, TGNP MTANDAO,HAWA NA OXFAM TANZANIA WAWAKUTANISHA WANAWAKE VIONGOZI KATIKA KUJADILI MASWALA YA KUMKOMBOA MWANAMKE KISIASA NA KIUCHUMI, SERENA JIJINI DAR.

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania Bi. Marry Lusimbi akitoa neno la utangulizi na kuwashukuru wanawake viongozi wote waliojumuika kwa pamoja katika Futari,na kujadili mambo ya msingi hasa ukombozi wa Mwaamke katika maendeleo,kisiasa,kiuchumi na jamii inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.
Dr. Eve Maria Semakafu,(wa katikati) akichangia jambo juu ya namna ya wanawake viongozi wanavyoweza kusaidia katika kuhakikisha wanafunzi wa kizazi cha sasa wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata elimu iliyobora na kubadili mfumo wa ufundishwaji kwani kwa sasa inaonekana wamekuwa wakidumaa sana kwa sababu ya kurahisishiwa kila kitu.
Bi. Fortunata Manyeresa(wa kwanza kushoto) akieleza namna mbalimbali za  kuwafikia wanawake ikiwa ni pamoja na njia ya Vikoba,pia alielezea namna wanavyofanya kazi kupitia Asasi  yao ya kiraia ya Tree of Hope yenye makazi yake Tanga
Bi. Eluka Kibona kutoka Oxfam Tanzania akielezea kwa undani maswala ya Siasa za ndani majumbani ambapo maana yake ni majukumu ya wanawake katika kulea familia zao majumbani bila malipo na kuongeza kuwa hayo yote yana mahusiano ya karibu baina ya matokeo ya uzoefu wa maisha ya wanawake na mfumo wa nchi ikiwa ni pamoja na Sera pia siasa.
Mmoja wa Viongozi wanawake Profesa Ruth Meena akieleza namna wanawake na wasichana wanavyopoteza muda mwingi katika kufanya kazi ambazo hazina malipo na kuwanyima kufanya kazi ambazo zingeweza kuwapatia kipato, alisema kupitia mkutano huu kunapaswa kuwa na maadhimio ambayo yatamsaidia mwanamke kuwa licha ya kufanya kazi za ndani lakini pia apate muda na wakufanya shughuli ambazo zitamsaidia kuingiza kipato
Mkurugezi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania Bi. Tike Mwambipile (Kulia) akichangia jambo wakati wa Futari hiyo ambapo alisema kuwa ushirikishwaji wa wanawake vijana katika ukombozi wa mwanamke katika kuleta maendeleo ni muhimu kwa kuwa wananguvu na wanatakiwa mwongozo bora na kuwasaidia katika mambo mengine ili waje kuja kuwa viongozi bora wa Baadae.
Happiness Maruchu kutoka TGNP Mtandao ambaye alijikita katika nafasi ya vijana katika kuhakikisha kwamba ukombozi wa wanawake kimapinduzi unakuwa ajenda kuu ya kitaifa huku usawa wa kijinsia ukiwa nguzo ya kufanikisha maswala hayo,na kuongeza kuwa wanawake vijana wanaweza kufanya mambo makubwa ya kuwakomboa wanawake wengi zaidi.
Irene Kiria kutoka HAWA akichangia jambo na kuwashukuru viongozi wote ambao walifika katika Futari kwa kuwa amejifunza mengi na ataenda kuyafanyia kazi zaidi katika kazi zake na aliongeza kuwa vyombo vya Habari ni muhimu sana katika kufikisha taarifa hizi juu ya ukombozi wa wanawake.
Bi. Jane Remme Kutoka Asasi ya kimataifa ya kiraia Oxfam akichangia jambo wakati wa jukwaa hilo.
Mkurugezi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bw. Francis Odokorachi (kulia) akizungumza na baadhi ya waliofika katika futari.
Kikao kikiendelea. 


Asasi za Kiraia za Women Fund Tanzania,HAWA,TGNP  Mtandao  na Oxfam Tanzania wamewakutanisha wanawake viongozi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ili kujadili namna ya ukombozi kwa wanawake ikiwa ni kisiasa,kijamii na kiuchumi na kuhaki kisha hiyo ndio inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.


Akizungumza kwa niaba ya Asasi zilizo andaa futari hiyo ya pamoja Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania  Bi. Mary Lusimbi alisema kuwa mjadala huo ulilenga kuwajenga viongozi hao kwenye mahusiano na ushirikiano wa wanawake kufungua nafasi kwa viongozi wanawake wengine kushiriki pamoja ili kuleta uwiano kijinsia .

"Tunaposema Masuala ya Siasa za Ndani Majumbani tunaongelea   majukumu ya Wanawake  katika kulea familia na nyumba bila malipo ukiwa na  maana  pana pia ni kwamba kuna mahusiano ya karibu  baina ya matokeo na uzoefu wa maisha ya wanawake na mfumo wa nchi, sera, na siasa.," alisema 

Wakati wa mjadala huo mpana wanawake hao viongozi waligusia kwa kina kuwa nguvu ya malengo ya ukombozi wa mwanamke  kisiasa, kijamii na kiuchumi itasukumwa kwa pamoja kutokana na umoja wa wanawake waliopo katika nafasi za uongozi kupitia nafasi zao binafsi,taasisi na taaluma zao.

Walisema kuwa katika jamii zetu kuna mila na desturi ambazo zinahusiana na jinsia zinazo onesha kwamba katika jamii nyingi wanawake na wasichana hufanya kazi za nyumbani za kuhudumia familia na kulea kwa muda mrefu zaidi kulipo wanaume kazi hizo ni pamoja na kutunza wazee pamoja , kulea watoto, kuhudumia wagonjwa, kuandaa chakula, kusafisha, kuchota  maji na kukusanya  nishati kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, na kuongeza kuwa Takwimu zinaonesha kwamba pato la taifa lingeweza kukuwa kati ya asilimia 10 hadi 39 endapo Serikali ingewekeza katika kazi za nyumbani zisizo na malipo.

Pia ili kufanikisha haya Makundi mbalimbali, Wadau na Serikali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo  ambayo ni pamoja na Kupunguza kazi za nyumbani zisizo na malipo kwa kuweka mifumo sahihi itakayo rahisisha na kupunguza muda, Kuzitambua kwa kuziweka katika mifumo ya kisera na kibajeti na pamoja na  Kuhakikisha makundi mbalimbali ya wanawake na wasichana yanapata uwakilishi katika  ngazi za maamuzi, Kugawanya  kazi hizi kwa makundi tofauti  na kwa uwiano unaofaa kati ya wanawake na wanaume, jamii na familia.
 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa