Na Thobias Robert.
Imebainika
kuwa ada kubwa inayotozwa na Chama cha Mawakili Tanganyika
(TLS),imekuwa kikwazo kwa wanachama kujiunga hivyo kukosa haki yao
msingi ya kuwa wanachama na hivyo kunyimwa haki ya kushikiri kwenye
chama chao cha kitaaluma.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Kujitegemea
ambaye pia ni Mwanachama wa chama hicho, Bwana Emmanuel Makene
alipokuwa akizungumza na Wandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es
Salaam kuhusu changamoto zinazoendelea ndani ya chama hicho.
“Mawakili
tunatumia zaidi ya milioni 2 hadi 4 kwa mwaka kwa ajili ya malipo
mbalimbali ya chama,ikiwemo ada ya uanachama, kuidhinishwa na Serikali
na kuhuisha leseni ya uwakili ya kila mwaka” alisema Makene.
Aidha
mawakili wanatakiwa kulipa ada ya uanachama wa Afrika Mashariki (EALS)
kiasi cha dola 50 za Kimarekani kila mwaka. Malipo mengine ambayo
mawakili wanapaswa kulipa ni pamoja na pesa za ujenzi wa jengo la chama
(Wakili House) ambapo ndani ya chama hicho hakuna mwanachama yeyote
mwenye hisa.
Pamoja na malipo makubwa ndani ya chama hicho,
Makene amesema kuwa chama hakina msaada wowote kwa mwanachama endapo
atapata tatizo lolote kama vile ugonjwa,jambo ambalo linawakwaza na
kuhoji pesa wanachanga za nini.
“Wakili ukiwa mgonjwa au upate
tatizo lolote chama hakitoi hata senti moja sasa hela tunachangia za
nini ,kiufupi hatufaidiki na chama chetu japo tunalipa pesa nyingi,”
alisema Wakili Makene.
Mbali na malalamiko ya kuwepo kwa michango
mingi, Bwana Makene alisema kuwa, chama kina hati chafu kutoka kwa
Mkaguzi wa Mahesabu ya Serikali ya mwaka 2015 ambapo chama kinatuhumiwa
kwa ubadhilifu wa fedha zaidi ya milioni 200.
“Kuna tuhuma za
ubadhilifu wa fedha za chama ambao umefumbiwa macho. Mkaguzi wa mahesabu
alionesha ubadhilifu mkubwa na akatoa hati chafu kwa TLS mwaka
2015,ambapo taarifa ya mkaguzi wa nje wa mahesabu ya TLS ameonesha zaidi
ya milioni 200 kuwa hazijulikani zilipo,” alisema wakili Makene
Pia
Wakili huyo alitoa wito kwa Mawakili na wadau wa sheria kutii sheria
na kujiepusha na kauli zinazoligawa taifa, “Tujitahidi sana kuchunga
kauli zetu hasa kuhusiana na jamii tunayoishi ili tusiwagawe watu
kidini, kikabila ama kiitikadi,na tukumbuke kuwa mawakili hatuko juu ya
sheria” alisema Makene
Hayo yamesemwa na Wakili wa Kujitegemea
ambaye pia ni Mwanachama wa chama hicho, Bwana Emmanuel Makene alipokuwa
akizungumza na Wandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es Salaam
juu ya malalamiko na changamoto zinazoendelea katika chama hicho.
“Mawakili
tunatumia zaidi ya milioni 2 hadi milion 4 kwa mwaka kwa kulipa kwenye
chama cha mwakili. Ada ya mwananchama kwenye chama cha TLS ni kubwa sana
kuliko taasisi za taaluma.
Chama cha Mawakili Tanganyika
kilianzishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1954 kwa lengo la kulinda na
kutetea masilahi ya mawakili Tanzania bara, kutoa elimu na msaada wa
kisheria kwa wananchi lakini pia kutetea na kusimamia masilahi ya
wanyonge nchini.
0 comments:
Post a Comment