Na. Georgina Misama – MAELEZO
Katika
hatua za kuunga mkono utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli,
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) imesema imeanza kuchukua
hatua za kuwawajibisha wafanyakazi wazembe na wasio waadilifu.
Akiongea
na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo
Jijini Dar nes Salaam, Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Bw. Gulamhafeez
Mukadamu alisema kwamba ili kurejesha imani iliyopotea kwa Wanajumuiya
wa ALAT, hatua mbalimbali za kinidhamu zitachukuliwa kwa baadhi ya
watumishi wa ALAT Makao Makuu.
“Katika
Mkutano wetu Mkuu wa Taifa wa 33, utakaofanyika Septemba 19, 2017,
tutatoa taarifa ya hatua zinazochukuliwa na zitakazochuliwa kwa
watumishi wa Sekretarieti ya ALAT Makao Makuu ambao siyo waadilifu na
wenye utendaji kazi usioridhisha ili kuweka mwelekeo mpya wa ALAT,”
alieleza Mukadamu.
Aidha,
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, kwa kuona umuhimu wa dhamira ya Serikali
ya Awamu ya Tano, ALAF inaunga mkono juhudi za Mhe. Rais za Serikali
kuhamia Dodoma, ambapo kuanzia tarehe Mosi Agosti mwaka huu ALAT nayo
itahamishia Makao Makuu ya ofisi zake Mjini Dodoma.
Bw.
Mukadamu pia alitumia wasaa huo kutoa taarifa ya Mkutano Mkuu wa 33 wa
Kawaida, unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu Jijini Mbeya na
kuhudhuriwa na takribani wajumbe 500. Mkutano huo utahudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Vitengo,
Wakuu wa Taasisi za Serikali za Mitaa na Maofisa kutoka Sekretarieti za
Mikoa.
Kwa
Mujibu wa Mukadamu, mkutano huo pia utahudhuriwa na wawakilishi wa
Wabia katika Maendeleo na Mabalozi, Jumuia za Serikali za Mitaa za nchi
za Kenya (ALGAK), Uganda (ULGA) na Rwanda (ABELO) pamoja na Asasi zisizo
za Serikali na Sekta binafsi.
Jumuia
ya Tawala ya Mitaa Tanzania ilianzishwa Mjini Dodoma, Desemba 1984
baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa Serikali za Mitaa kwa lengo la
kuwakilisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa inayoziunganisha Halmashauri za
Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment