Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » BARABARA YA SARANGA-KING'ONG'O KUKARABATIWA KWA DHARULA

BARABARA YA SARANGA-KING'ONG'O KUKARABATIWA KWA DHARULA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiwa ameongozana na kamati ya fedha wakikangua barabara ya Saranga, King'ong'o ambazo zipo kwenye Matengenezo ya dharura, jijini Dar es Salaam.
Dereva wa pikipiki akikwepa shimo katika barabra ya Saranga, King'ong'o jijini Dar es Salaam.


Halmashauri ya manispaa ya Ubungo, kupitia ziara ya kamati ya fedha iliyokuwa ikiongozwa na Mstahiki Meya, Boniface Jacob walifika kujionea hali ya uharibifu wa barabara hasa maeneo ya Kwandevu kuelekea King'ong'o kata ya Saranga.
Nakuhaidi kuishughulikia kwa dharula maeneo mawili 

yaliyoonekana kuharibika sana na kisababisha uharibifu wa magari, foleni na kuhatarisha Maisha ya watembea kwa miguu.

Matengenezo ya dharula yataanza hivi karibuni chini ya Mhandisi wa Halamshauri ya Ubungo huku Manispaa ikiendelea kufuatilia kuingiziwa fedha za barabara hiyo kutoka Manispaa ya kinondoni kwenye akaunti ya pamoja iliyofungwa na Bodi ya barabar ambapo zilitengewa kiasi cha shillingi Millioni 400 kuweka zege maeneo yote ya miteremko na vilima vya Matosa mpaka kimara kupitia King'ong'o.
IMETOLEWA Na OFISI YA MSTAHIKI MEYA HALMASHAURI YA MANISPAA UBUNGO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa