Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KAMATI YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKUTANA NA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA BIASHARA HIYO

KAMATI YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKUTANA NA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA BIASHARA HIYO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella, akizungumza na wadau kutoka taasisi zinazojihusisha na kupambana na biashara hiyo waliokutana katika jijini Dar es Salaam leo, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo nchini. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa uchunguzi Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Ahmed Mwendadi, akifafanua jambo kwa wadau kutoka Taasisi zinazopambana na biashara hiyo waliokutana jijini Dar es Salaam, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ANPPCAN Tanzania, Wilbert Muchunguzi, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa