Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAHAKAMA YAIAMURU MAGEREZA KUMPELEKA HOSPITALI KWA MATIBABU MSHTAKIWA HARBINDER SINGH

MAHAKAMA YAIAMURU MAGEREZA KUMPELEKA HOSPITALI KWA MATIBABU MSHTAKIWA HARBINDER SINGH

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru Magereza kumpeleka mshitakiwa Harbinder Singh Sethi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu. 

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema hayo leo, baada ya mshtakiwa Sethi kuieleza mahakama kuwa, anaumwa.

Hakimu Shaidi amesema,suala la afya ya mshitakiwa ni la msingi hivyo mamlaka zinazohusika zihakikishe mshitakiwa anapata matibabu na tarehe ijayo watoe taarifa kama amri imetekelezwa au la.

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo, mshtakia Seth amedai kuwa hali yake ni mbaya kwani aliongea  na magereza ili aweze kupata matibabu toka kwa daktari wake lakini alipelekwa Hospitali ya Amana.

Sethi amedi kutokana na maradhi yake ya uvimbe tumboni kuhitaji mtaalamu, alishindwa kupata matibabu katika hospitali ya Amana.

Mwendesha Mashitaka kutoka  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Vital Peter alidai suala la ugonjwa ni la kitaalamu ambalo linahitaji kuthibitishwa ili kujiridhisha licha ya mshitakiwa kujieleza, hakuna nyaraka zinazounga mkono hoja zake kutoka kwa mtaalamu zinazoelezea hali yake.

Alidai kutibiwa ni haki ya mshitakiwa kwa kuwa wapo wataalamu katika hospitali  ya Muhimbili na magereza.

Hata hivyo, alidai upelelezi wa shairi hilo haujakamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kutajwa.

Sethi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP), anashtakiwa na mwenzake,  James Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL).

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni 22. 1 na Sh bilioni 309.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia upelelezi umefikia wapi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa