Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MBUNGE WA TEMEKE AHUKUMIWA KWA KUENDESHA GARI BILA BIMA NA KUTOTII AMRI YA POLISI

MBUNGE WA TEMEKE AHUKUMIWA KWA KUENDESHA GARI BILA BIMA NA KUTOTII AMRI YA POLISI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mbunge wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea jana alipandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashataka mawili ikiwemo la kuendesha gari bila ya bima kinyume na sheria za nchi.

Mbunge huyo kwa tiketi ya chama cha wanachi CUF, alisomewa mashtaka yake mbele ya hakimu mkazi Mhe. Eliarusia Nassatri mbale ya mwendesha mashtaka wa serikali Joseph Maugo ambaye aliiambia mahakama hiyo kuwa katika kosa la kwanza Mbunge huyo anadaiwa kuendesha gari ambalo halina bima

Maelezo ya kosa hilo yanadai kuwa, Julai 19 mwaka huu katika barabara ya Kilwa eneo la Bendera tatu, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 672 BNV Toyota Mark 2 likiwa halina bima.

Katika kosa la pili, mshatakiwa Mtolea anadaiwa kulitenda muda na eneo la kwanza alipotenda kosa la kwanza kwakushindwa kutekeleza agizo la ofisa Polisi mwenye namba F 818 Kopla Robati la kutakiwa kupeleka gari hilo katika kituo cha Polisi Kilwa Road lakini mshtakiwa alikaidi agizo hilo na kuelekea maeneo ya katikati ya jiji.

Baada ya kusomewa makosa hayo, Mtolea alikiri makosa yote ambapo alisomewa maelezo ya awali (PH) kisha kuhukumiwa kulipa faini ya Pound 100 na Tsh. 30,000.

Katika hukumu yake, Hakimu Nassary alisema, kosa la kwanza mshtakiwa anatakiwa kulipa Pound 100 sawa na Tsh. 291,700 au kifungo cha miezi 6 jela wakati kosa la pili ni kulipa faini ya Tsh. 30,000 au kifungo cha miaka 2 jela ambapo baada ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Hashim Mziray aliieleza kuwa mteja wake atalipa faini hiyo.
 
Chanzo Vijimambo Blogu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa