Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali
imeeleza kuwa inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na
Vyombo vya Habari nchini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa
sahihi na kwa wakati.
Akizungumza katika ziari yake alipotembelea
vyombo vya habari vya Radio EFM na Radio One/ ITV leo Jijini Dar es
Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuwepo kwa
ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.
“Lengo la ziara hii
ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na
kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi
vyenu mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel
Aidha aliongeza kuwa
ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya
habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa
mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa
letu.
Kwa upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa
vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na
uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Pia amewataka
watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni wa kufanya kazi
kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na
kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye
usahihi.
Sambamba na hilo Prof. Gabriel amevitaka vyombo hivyo
vya habari kuzingatia maudhui yanayoendana na jamii ya kitanzania pale
wanapoandaa vipindi mbalimbali ili kujenga jamii yenye utamaduni mzuri
ikiwemo kufanya kazi kimkakati.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Redio Efm, Bw. Denis Ssebo amesema kuwa uongozi wa radio yake upo
tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali lengo likiwa ni
kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za utangazaji ili kufanya kazi
kwa kiwango chenye ubora .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Radio One/ITV Bibi. Joyce Mhaville ameishukuru serikali kupitia wizara
ya Habari kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na vyombo vya habari ikiwemo
kufanya kazi kwa karibu na kuviwezesha vyombo hivyo kupata habari
zenye ukweli na uhakika.
0 comments:
Post a Comment