Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, amekamatwa na Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa tisa.
Kwa
mujibu wa Gazeti la Mtanzania, Sheikh Khalifa alifika Kituo Kikuu cha
Polisi Dar es Salaam jana saa nne asubuhi na kuhojiwa kwa muda mrefu,
huku ikiwa haifahamiki hasa sababu za kushikiliwa kwake.
Taarifa
zilizopatikana jana jioni zilidai kuwa polisi walikuwa wamepanga
kumchukua sheikh huyo kwa ajili ya kwenda kupekua nyumbani kwake. Hata
hivyo hadi saa mbili usiku alikua bado anashikiliwa polisi.
Kwa
nyakati tofauti jana Sheikh Khalifa mwenyewe aliliambia gazeti la
Mtanzania kuwa alipofika kituoni alielezwa na polisi kwamba ameitwa
kuhojiwa kuhusu tuhuma za uchochezi.
Alisema
kwamba alihojiwa kuhusu kuunga mkono kauli ya Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, juu ya masheikh wa uamsho na hatua yake ya kuwataka
waumini wa dini ya kiislamu kuungana kutetea haki za Waislamu waliopo
katika magereza mbalimbali nchini.
“Wameniuliza
mambo ya kumuunga mkono Lowassa na pia waliniuliza kwanini niliwataka
Waislamu nchini kuungana kuwatetea Waislamu waliopo kizuizini kwa makosa
ya kubambikwa.
“Hadi sasa niko hapa polisi bado nasubiri ni nini kitaendela kama wataniachia au watanibakisha hapa hatujajua,” alisema.
Alichosema Sheikh Khalifa
Baadhi ya mambo aliyoyasema Sheikh Khalifa katika mkutano wake na waandishi wa habari jumapili ya wiki hii.
“Tunaiomba
Serikali iweke wazi kwa nini hairuhusiwi kwa sheikh au mtu yeyote
aliyewekwa ndani gerezani kuonwa na zaidi ya mtu mmoja hadi siku 14
zipite, yaani akija mkewe au ndugu yake leo kuonana naye ipite siku 14
ndio aje ndugu yake mwingine kumuona hayo mambo hayapo na hayamo katika
sheria.
“Tunampongeza
Lowassa kwa kuona kwamba jamii miongoni mwa Watanzania inadhalilika na
haitendewi haki na kama yeye aliyasema maneno haya kwa kutafuta faida
za kisiasa hayo ni maneno yake lakini aliyoyasema ni haki na kweli,”
alisema sheikh Khalifa.
Kauli ya Lowassa
Akiwa
katika futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Lowassa
alitaka serikali iharakishe kesi za masheikh wa uamsho na kama baadhi
yao hawana makosa waachiwe huru.
Alisema
wakati wa kampeni za mwaka 2015, alitoa ahadi nyingi ikiwa ni pamoja na
kupitia upya mikataba ya madini, pamoja na kuwaachia masheikh wa uamsho
hivyo kama Rais John Dk. Magufuli amefanyia kazi la madini, afanye
hivyo pia kwa masheikh hao.
0 comments:
Post a Comment