Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TUNDU LISSU AKAMATWA AKIWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA KWENDA RWANDA

TUNDU LISSU AKAMATWA AKIWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA KWENDA RWANDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amekamatwa, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martin Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi kwa ma.
Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.
Nae Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amekiri kuwa mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa