Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UTALII WAZIDI KUONGEZA PATO LA TAIFA

UTALII WAZIDI KUONGEZA PATO LA TAIFA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Na Thobias Robert.
Sekta ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka huu wa fedha.
Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa maendeleo ya watanzania wote.
Mkurugenzi huyo wa TANAPA alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 TANAPA ilichangia kiasi cha billion 27 kwenda Mfuko wa Taifa wa serikali na matarajio yao katika kuchangia mfuko wa fedha wa Taifa kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni bilioni 33.4 hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa Watalii kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
Kuongeza kwa watalii hasa katika hifadhi za Taifa kunatokana na TANAPA kujitangaza zaidi katika nchi mbalimbali duniani kupitia Mitandao ya kijamii, Makampuni binafsi ndani na nje ya nchi, Balozi za Tanzania katika mataifa ya Nje, Vilabu mbalimbali vya Ulaya na Amerika pamoja Vyombo vya Habari vya kimataifa kama vile CNN na BBC.
Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri, hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini ndiyo sababu zinazowavutia watalii kuongezeka kila mwaka.
Pamoja na kukua na kuongezeka kwa utalii nchini kunakopelekea kuongeza la Taifa, Mkurugenzi Kijazi alisema kuwa, utalii wa ndani bado ni changamoto kwani watalii wengi wanatoka nje ya Nchi huku wazawa wakishindwa kuzuru maeneo mbalimbali ya utalii ili
kujionea fahari ya nchi yao hivyo ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ili kukuza na kuongeza pato la Taifa.
Hivi karibuni Mtandao wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii barani Afrika uliitaja Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za watalii barani humu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa