Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wasichana
wanachama wa Tanzania Girl Guides wakiwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakitokea kwenye ziara ya
programu ya miezi sita ya mafunzo ya kubadilisha uzoefu katika masuala
ya utamaduni, uongozi na maadili. Kutoka kushoto ni Ummy Mwabondo
alikwenda Zambia, Edna Chembele (Zimbabwe), Elizabeth Betha (Madagascar)
na Farida Mjoge aliyekuwa Uganda. PICHA, HABARI NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
WASICHANA
wanne wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) wamerejea
nchini kutoka kwenye programu ya mafunzo ya miezi sita katika nchi
mbalimbali za Afrika.
Wasichana
hao waliokuwa kwenye mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika mambo ya
utamaduni, uongozi na maadili katika nchi za Zambia, Zimbabwe,
Madagascar na Uganda wameipongeza TGGA kwa kufanikisha ziara hiyo yenye
mafanikio makubwa katika maisha yao.
Walipowasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana kwa
ndege ya Kenya Airways, walilakiwa na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba,
ndugu jamaa na marafiki huku wengine wakivishwa mashada na kupatiwa
zawadi mbalimbali. Wasichana waliokwenda kwenye mafunzo hayo ni; Ummy
Mwabondo, Elizabeth Betha, Edna Chembele na Farida Mjoge ambao kila
mmoja anaeleza jinsi alivyonufaika na ziara hiyo.
Elizabeth
Betha ambaye programu yake aliifanyia Madagascar, anaeleza kuwa
Wananchi wa Kisiwa hicho utamaduni wao ni tofauti kabisa na wa Tanzania
na maeneo mengine ya Afrika, ambapo mara nyingi hutumia lugha yao ya
asili na kifaransa kama Lugha yao ya Taifa, ni wakarimu sana na wana
upendo.
Anasema
kuwa licha ya kuwafundisha mambo mengi ya Tanzania ikiwemo utamaduni,
mapishi ya vyakula mbalimbali, lugha ya kiswahili na vivutio mbalimbali
vya kitalii pia wakiwa huko walipanda miti, kufundishana kwa uwazi
masuala ya hedhi salama, kuzuia ukatili wa kijinsia pamoja na kuwapa
stamina ya kujiamini na kujithamini.
0 comments:
Post a Comment