Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATUMIAJI WA USAFIRI WA ANGA

WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATUMIAJI WA USAFIRI WA ANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


 Mkurugenzi  Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari, akitoa mada kuhusu wajibu wa Mashirika ya Ndege kwa Abiria Kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu Kuhusu Namna ya Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga Nchini Iliyofanyika Morogoro, Kuanzia Julai 20, 2017. 

 Washiriki wa Semina kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya matumiaji wa Usafiri wa Anga wakifuatilia mada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC) Elias Mwashiuya, akiwasilisha mada kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Julai 20, 2017.



Wataalam wa Usafiri wa Anga nchini wamekutana katika semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kushughulikia malalamiko na kero za watumiaji wa usafiri wa anga nchini katika semina iliyofanyika mjini Morogoro kuanzia Julai 20, 2017

Semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) nchini imewakutanisha wajumbe wa kitengo cha Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga cha TCAA(TCAA-CCU), Watendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC), wanasheria wa Mamlaka na maafisa kutoka idara ya udhibiti masuala ya Kiuchumi ya TCAA ambayo inajukumu la kulinda maslahi ya watumiaji wa usafiri wa anga .

Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na wajibu wa kampuni za ndege kwa abiria, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza S. Johari, majukumu ya kitengo cha kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga na nyezo za kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga.

Semina hii ni sehemu ya mkakati wa usafiri wa anga wa kuboresha huduma zinazotolewa kwa watumiaji wa usafiri wa anga na kukuza sekta ya usafiri wa anga Tanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa