Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA VYUO VIKUU, ATAKA PROGRAMU ZA ELIMU YA JUU ZIWEZESHE WAHITIMU KUJIAJIRI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA VYUO VIKUU, ATAKA PROGRAMU ZA ELIMU YA JUU ZIWEZESHE WAHITIMU KUJIAJIRI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu mtambo wa kuamia ndege waharibifu wa mazao kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Tekinolojia ya Dar es salaam (Dar es salaam Insititute of Technology), Profesa Preksedis Ndomba (kulia) wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea mabanda kabla ya kufungua Maonyesho ya Vyuo Vikuu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia kwake) pamoja na Viongozi wa TCU wakiimba wimbo wa taifa kabla ya Waziri Mkuu kufungua Maonyesho ya Vyuo Vikuu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dr es salaam Julai 26, 2017.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha kwamba programu zote zinazotolewa na taasisi za elimu ya juu zinawawezesha wahitimu kujiajiri na kuwa na sifa za ushindani katika soko la ajira kimataifa.

Amesema wakati umefika sasa kwa wasomi katika vyuo vyetu vikuu tujiridhisha kuwa mitaala inayotolewa kama inawaandaa wahitimu kupata taaluma na stadi za kuweza kujiajiri na kupambana na changamoto za kimaisha.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 26, 2017) wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya Elimu ya Juu, jijini Dar es Salaam.  Amesema taasisi za elimu ya juu nchini ziangalie mitaala yake na kuimarisha mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ili kwenda sambamba na dunia ya kazi inayoendana na agenda ya maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu amesema maonesho hayo ni jukwaa la kipekee ambalo litaibua mjadala sahihi kuhusu uhalali wa kozi zinazotolewa na vyuo husika vya elimu ya juu. “Hivyo mnayo nafasi ya kuonesha kwa vitendo uwezo wenu katika utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia zinazotumika katika maendeleo ya viwanda.”

Amesema ni vema mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ukaimarishwa ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada kwenye sekta ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.

Amesema taasisi za elimu ya juu ziweke mikakati ya kuinua na kuboresha taaluma  wanayoitoa ili ilete tija kwa maendeleo ya Taifa na Dunia. Pia kuanzisha program za mafunzo zenye kukidhi mahitaji na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi hizo kuendelea kuimarisha mfumo wa udahili na kujipanga kutumia fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya nchi kwa makundi yote ya jamii kwa usawa katika ngazi zote hususan ufundi, hisabati, sayansi na teknolojia.

Pia Waziri Mkuu amesema ni wakati muafaka kwa taasisi za elimu ya juu nchini kuandaa mikakati ya kuongeza udahili kwa kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu na ujuzi unaohitajika katika sketa zinazokua haraka mfano mafuta, gesi na madini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa