Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mshambuliaji
wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na
wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye
Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Kocha
George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani
katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini
Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kikosi cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina.
Yanga waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki moja na nusu ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.
Leo mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.
Mechi ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment