Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » BANDARI, POLISI NA UHAMIAJI WATAKIWA KUKAGUA MIZIGO YOTE YA ABIRIA BANDARINI

BANDARI, POLISI NA UHAMIAJI WATAKIWA KUKAGUA MIZIGO YOTE YA ABIRIA BANDARINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
video

Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Jeshi la Polisi kikosi cha Bandari pamoja na Jeshi la Uhamiaji wametakiwa kuhakikisha wanakagua abiria na mizigo yote inayopita katika bandari zote nchini ili kuhakikisha abiria na mizigo yote inafuata taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa sheria jambo ambalo litaimarisha usalama bandarini. 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun katika ziara ya kukagua namna watalii wanavyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam. 
Katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhandisi Ramo Makani na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema ni muhimu kuweka takwimu vizuri za watalii wanaopita katika bandari zote ili kujua idadi kamili ya watalii wanaokuja kwa kutumia njia ya maji. 
Akielezea jinsi wanavyowapokea watalii wanaokuja kwa meli katika bandari ya Dar Es Salaam, Meneja wa Operesheni amesema wamekuwa wakikutana na wadau kila siku ili kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya ujio wa watalii nchini. Manaibu Waziri hao pia walitembelea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal II na kukagua ujenzi wa Terminal III unaoendelea. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa