Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWAAHIDI BFT KUWATATULIA KERO YA ENEO LA MAFUNZO

DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWAAHIDI BFT KUWATATULIA KERO YA ENEO LA MAFUNZO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha Jarida la Mpango Mkakati la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) mara baada ya kufanya nao mazungumzo katika Ofisi za Wizara 01 Agosti, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaana Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) kuwatatulia kero ya eneo la kufanyia mafunzo pamoja na ofisi ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu zikiwemo na changamoto nyingine za Shirikisho hilo.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo ikiwa ni sehemu ya kutambua utendaji kazi wao na changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.

Dkt. Mwakyembe amesema kwamba, kutokana na tatizo la ukosefu wa eneo rasmi la ofisi na sehemu ya kufanyia mafunzo, yeye atawasiliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili kuona namna gani wanaweza kupata eneo kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kwa ajili ya kujenga ofisi na eneo la kufanyia mazoezi.

Sambamba na hilo, ameupongeza uongozi wa shirikisho hilo kwa kazi wanazozifanya na kuwataka wazidi kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hususani katika kupeana taarifa zinazohusu maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.

“BFT jitahidini muwe na ushirikiano wa karibu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na msifanye mambo yenu kimya kimya, muwasiliane kwa karibu na BMT kwani hii itasaidia Wizara kushughulikia kero zenu mbalimbali kuliko mkichelewa kutoa taarifa mapema”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, amewahakikishia kuwa, yupo tayari kutafuta wafadhili ndani na nje ya nchi ili waweze kulisaidia shirikisho hilo kutatua kero za uhaba wa vifaa, rasilimali fedha pamoja na ukosefu wa mafunzo kwa makocha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amelitaka shirikisho hilo kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali ikiwemo kujenga tabia ya ulipaji kodi, kuwaelimisha Wanamasumbwi kuachana na tabia chafu wanapokuwa michezoni pamoja na kuachana na kujihusisha na madawa ya kulevya.

Kwa upande wao Viongozi wanaounda shirikisho hilo pamoja na wajumbe kwa pamoja wamemuahidi Waziri Mwakyembe na Wizara kwa ujumla kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuboresha suala la mawasiliano kati ya Shirikisho na Wizara, kufuatilia suala la mikataba mbalimbali na uwajibikaji yakinifu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa