Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » HOSPITALI YAKABILIWA UHABA WA WODI DAR ES SALAAM

HOSPITALI YAKABILIWA UHABA WA WODI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

HOSPITALI ya Mbagala Zakhem iliyopo jijini Dar es Salam, inakabiliwa na uhaba wa wodi za kulaza wagonjwa pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti kwa muda mrefu.

Mbali na changamoto hiyo, pia hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi baada ya wafanyakazi 16 kuondolewa katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Joseph Kiani, aliyasema hayo wakati akipokea msaada wa mabenchi ya kukalia 30 na sabuni ndoo 40 vyenye thamani ya Sh. milioni 12 kutoka kampuni ya Good One.

“Msaada huu utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hii, lakini kuna changamoto nyingi kama vile kutokuwapo kwa wodi ya watoto na wodi ya wazee,” alisema Dk. Kiani.

Dk. Kiani alisema kwa sasa hospitali hiyo ina wodi moja ya kinamama, hali inayosababisha kushindwa kuwalaza wagonjwa wengine.

Alisema kupitia msaada huo utasaidia kutatua changamoto ya idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kukosa mabenchi ya kukalia.

Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Hashim Komba, alishukuru kwa msaada huo na kutoa wito kwa taasisi na watu binafsi kuona umuhimu wa kusaidia.

Alisema maendeleo ya Wilaya ya Temeke yataletwa na kila Mtanzania kwa kushirikiana.

Mmoja wa wagonjwa katika hospitali hiyo, Mwantumu Juma, alisema msaada huo utawawezesha wagonjwa kujisikia faraja wanapofika katika hospitali hiyo kwa sababu awali walikuwa wanakosa mahali pa kukaa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa