Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KULIKO KITHIRI SHERIA MKONONI

KULIKO KITHIRI SHERIA MKONONI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, PICHA: JOHN BADI

JIJI la Dar es Salaam linaongoza kwa matukio ya mauaji yatokanayo na watu kujichukulia sheria mkononi, imeelezwa.
Imeelezwa kuwa jijini Dar es Salaam palikuwa na mauaji yaliyofikia 117 katika kipindi cha nusu mwaka.

Hayo yamo kwenye Ripoti ya utafiti iliyotolewa jana jijini na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kuhusu haki za binadamu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, alisema haki ya kuishi ni miongoni mwa haki zinazokiukwa kama vile watu kufia mikononi mwa vyombo vya dola, imani za kishirikina na ubakaji.

Pia alisema kati ya matukio 479 yaliyotokea katika kipindi hicho nchini, mauaji 117 yalitokana na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, ikifuatiwa wa mikoa ya Mbeya (33), Mara (28) na Geita (26).

Aidha, Dk Kijo-Bisimba alisema kati ya ajali 3,090 zilizosababisha vifo 1,308, vifo 126 vilitokea Dar es Salaam, ikifuatiwa na Mbeya (73), Tabora (61) na Arusha (69) likiwamo tukio la ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu na dereva wa shule ya St. Lucky Vincent.

Aidha, Bisimba alisema matukio ya ubakakaji yaliyotokea kipindi hicho yameongezeka Mara mbili, huku Mkoa wa Iringa ukiwa kinara wa matukio ya kubaka.
Alisema matukio 2,059 ya ubakaji yaliyoripotiwa Januari hadi Juni mwaka huu ni mengi ikilinganishwa na matukio 2,859 yaliyotokea mwaka mzima wa 2016.

"Iringa ubakaji uko juu, kwa nusu mwaka tu watoto 121 wamebakwa, wamenajisiwa na kulawitiwa huku wengi wao wakifanyiwa na ndugu wa karibu kama, mjomba, kaka, baba mama babu," alisema Bisimba.

Pia utafiti huo ulibaini kuwa Mkoa wa Tabora unaongoza kwa matukio ya mauaji ya imani za kishirikina kwa kuwa na vifo 23 kati ya 115 yaliyoripotiwa vituo vya polisi nchini.
"Mauaji yanayohatarisha amani na usalama ni yale yaliyotokea maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji ambao watu 40 wakiwamo askari 13 waliuawa na watu wasiofahamika," alisema.

Alibainisha kuwa licha ya Tanzania kutotekeleza adhabu ya hukumu ya kifo, katika kipindi cha miezi sita, tayari watu saba wamehukumiwa adhabu hiyo na kwamba ni wakati kwa serikali kufuta adhabu hiyo ambayo haijatekelezwa tangu mwaka 1994.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa