Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
KaimuJajiMkuuwa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya. KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
Na Lydia Churi-Mahakama
Mahakama
ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa
haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri
Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa
miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto
kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.
UtekelezwajiwahakizaWatoto
zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa
nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba
21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za
watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni,
Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court)
katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili
hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es
salaam.
Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto
Kwa
kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya
Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa
(UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za
watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya.
Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama
ya watoto pekee kwa Tanzania bara.
Akizindua
jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa
mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye,
itakuwa hatarini.
0 comments:
Post a Comment