Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government
electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa
mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa
unatumika.
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Na; ELIAFILE SOLLA
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa
kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana
na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi
kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia
tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG,
utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa
kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila
kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio
ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio
makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi
katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo
kuhamishiwa mikoani.
Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au
shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi
kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa
kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa zile huduma nyingine za
sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika
daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea
ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio
ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha
kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa
kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza
kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa
Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi
katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji
kodi ya pango la ardhi nchini,
0 comments:
Post a Comment