Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAREHEMU PROFESA JOSEPH NAGU KUZIKWA ALHAMISI NYUMBANI KWAKE ENDASAKI, WILAYANI HANANG

MAREHEMU PROFESA JOSEPH NAGU KUZIKWA ALHAMISI NYUMBANI KWAKE ENDASAKI, WILAYANI HANANG

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Marehemu Profesa Joseph  Nagu,  aliyekuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Mzumbe, alikuwa  mume wa Mbunge wa Hanang- Mhe. Mary Nagu ambaye pia alikuwa Waziri katika serikali ya awamu ya tatu na ya nne. Marehemu Prof. Nagu ni baba wa Dr. Tumaini, Neema na Deogratias. 
Tunapenda kuwajulisha kuwa Marehemu atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwake Endasaki Wilaya ya Hanang siku ya Alhamisi tarehe 3/8/2017 
Leo saa kumi jioni Ibada ya kumuaga Marehemu imefanyika katika kanisa Katoliki St Peters Oysterbay jijini Dar es salaam kabla ya mwili kupelekwa kulala nyumbani kwake Regent Estate Mikocheni tayari kusafirishwa siku ya tarehe 02/07/2017 kuelekea Manyara, Hanang', Kijiji cha Endasaki. 

Raha ya milele umpe ee Bwanana na mwanga wa milele umwangazie.
Apumzike kwa Amani Mzee wetu Prof Joseph Nagu - AMEN.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa