Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MGAHAWA WA PIZZA HUT WAZINDULIWA MLIMANI CITY NA OYSTERBAY JIJINI DAR LEO.

MGAHAWA WA PIZZA HUT WAZINDULIWA MLIMANI CITY NA OYSTERBAY JIJINI DAR LEO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkurugenzi Mkuu wa Pizza Hut Afrika, Ewan Devenpot(Katikati) kwa pamoja wakishangilia mara baada ya kukata  utepe kufungua Mgahawa wa Pizza Hut Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai pamoja na Meneja masoko wa Pizza Hut Tanzania,Bahati Komba.
Sehemu husika kwa wahusika watakaotembelea Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa  ajira zilizopo ni katika viwanda vya mabox ambayo nao hutumia katika kuandaa Pizza pamoja na viwanda vya chill source, Tomato source ambapo kuna watu ambao wameajiliwa katika viwanda hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai na baadhi ya wateja wakionja pizza zilizoandaliwa ikiwa kunapizza za nyama, mbogamboga pamoja na uyoga.
 
Pizza Hut inamilikiwa na kampuni ya Dough Works Ltd, sasa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ambao ni watanzania hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Pizza Hut, Vikram Desai wakati wa uzinduzi wa  migahawa miwili iliyopo Mlimani City na Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

akizungumza katika uzinduzi wa migahawa hiyo amesema kuwa Mwaka huu mgahawa wa Pizza Hut ulitambulisha usambazaji bure wa chakula katika ofisi na majumbani na hivyo kuwarahisishia huduma wateja wake.
Migahawa miwili ya Pizza hut ipo katika eneo la maduka la Mkuki, jengo la Peugeot na Shoppers Plaza Mikocheni inaendelea kuhudumia mamia ya wananchi kwa chakula cha mchana na usiku.

Migahawa ya Pizza Hut ni ya kisasa ikiwa na sehemu ya watoto ya michezo mbalimbali, na sehemu za kukaa za ndani na nje. Pamoja na kuwa na chakula kitamu aina ya Pizza pia wametambulisha aina mbali mbali za bidhaa za kuku zenye ladha tofauti.

Zaidi ya mpango huo wa kupanua biashara kwa migahawa miwili zaidi kabla ya mwisho wa mwaka pia tunaangalia uwezekano wa kufungua biashara katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa