Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MWAKYEMBE ATAKA KUANZISHWA KWA MFUKO WA WASANII

MWAKYEMBE ATAKA KUANZISHWA KWA MFUKO WA WASANII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa mkutano wake na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TUMA Bw. Bryton Kibwana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo. Mkutano huo umeratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa lengo la kuwakutanisha wasanii hao na Mhe. Waziri ili kujadilia changamoto zao.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bw. Onesmo Kayanda akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Joyce Hagu akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Mkutano huo umewakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton) akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Mkutano huo umewakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo  na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Bw. Onesmo Kayanda wakati wa mkutano baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiteta jambo  na Katibu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton) wakati wa mkutano baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. 
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Jeff Mduma akitumbuiza wakati wa mkutano wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia) na wadau wa sanaa ya muziki leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kuwakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA). 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) na Kaimu wakipokea zawadi ya Saa ya Ukutani kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton)  ikiwa ni kutambua mchango wa Serikali katika kushughulikia changamoto za wasanii leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA). Kulia kushoto kwa Waziri ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bw. Onesmo Kayanda  na Msanii Witness Mwijage.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliochaguliwa kuwawakilisha wenzao katika kamati itakayoundwa na Serikali kwa ajili ya kupitia Sera na Sheria za sekta ya sanaa hapa nchini wakati wa mkutano na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Witness Mwijage, Azma Mponda, Taji Liundi na Nikki wa Pili.
Picha ya pamoja

Na. Neema Mathias na Thobias Robert- MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewahamasisha Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini kuanzisha mfuko wa wasanii kwa lengo la kutatua changamoto ya udhamini inayowakabili.
Waziri Mwakyembe ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wasanii hao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ambacho kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii na namna ya kukabiliana nazo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mwakyembe alisema kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo kutegemea wadhamini.
“Ninafikiri dawa tunayohitaji ni kuanzishe mfuko wa Wasanii ambapo kila Msanii atatakiwa kuchangia fedha. Jambo ambalo litawavutia wadau wengine kuchangia mfuko huo na kuwaondoa katika dhana ya utumwa, na mfuko huo utamsaidia msanii aliyejisajili kupata mkopo bila kutozwa riba yoyote,” alielezea Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya Sanaa ina mchango mkubwa katika kuongeza pato taifa hivyo ametaka tasnia hiyo kurasimishwa ili kupunguza tatizo la ajira na pia kutumika kama chombo maalumu cha kuielimisha jamii kwani kupitia Sanaa wananchi hupata ujumbe kwa urahisi.
Aidha, Waziri Mwakyembe ameunda Kamati ya kushughulikia masuala yanayowakabili Wasanii ikiwemo sera na sheria ili kuboresha maslahi ya Msanii. Wasanii wanaounda Kamati hiyo ni Azma Mponda, Niki wa Pili pamoja na Witness Mwaijanga.
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanyia mabadiliko sera ya Sanaa pamoja na baadhi ya vipengele vya sheria ya Sanaa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Tunahitaji mabadiliko ya sheria ya sanaa haraka. Katika sheria hiyo ni marufuku mmiliki wa vyombo vya habari kulipwa na Msanii ili kupiga wimbo wake, hakuna nchi katika dunia hii ambayo Msanii anatozwa fedha ili wimbo wake upigwe,” alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Onesmo Kayanda amesema kuwa, ili kuboresha na kukuza tasnia ya muziki nchini ni lazima kuwepo na soko la uhakika la kazi hizo pamoja na tuzo mbalimbali ambazo zitatumika kutia hamasa kwa wasanii. 
Hata hivyo Bw. Kayanda ameongeza kuwa sera, sheria na miongozo ya baraza hilo ihuishwe ili kulinda kazi mbaimbali za Wasanii ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kielektoniki wa kujisajili ili Serikali iweze kupata mapato halisi kupitia biashara ya muziki.
Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu Waziri Mwakyembe ateuliwe katika Wizara hiyo ambapo ameeleza kuwa kikao kazi kitakuwa kikifanyika mara kwa mara na atakuwa akikutana na wasanii wa vikundi mbalimbali ili kujadili mambo yanayohusu Wasanii hao. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa