Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NMB YAWEZESHA WAKUNGA MUHIMBILI KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE

NMB YAWEZESHA WAKUNGA MUHIMBILI KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
. Afisa Muuguzi Mwandamizi, Gudila Mambacho (kushoto) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa wananchi (kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Muuguzi mwandamizi na afisa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dotto Msabila Kafulie (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Maofisa Wauguzi na wataalam wa Kisukari Swaumu Gulumo na Sarah Mwakilima wakimuhudumia mmoja wa wananchi (kushoto) waliojitokeza kupima magonjwa mbalimbali bure katika kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wakunga duniani.. Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (aliyeshika kipaza sauti) akizungumzia huduma mbalimbali ya NMB kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma anuai za afya bure zilizokuwa zikitolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Afisa Muuguzi Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Janeth Mwambona (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.  
  Maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) wakimfungulia akaunti mmoja wa wateja (kulia) aliyejitokeza kupata huduma hizo katika kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Sehemu ya wananchi wakiwa katika foleni kupata huduma za afya bure zilizokuwa zinatolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo


 CHAMA cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB kimetoa huduma za afya mbalimbali bure jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. 

 Akizungumza leo na mwandishi wa habari hizi katika tukio hilo linaloendelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jirani na jengo la watoto, Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wakunga Tanzania tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Elizabeth Thawe aliwataka wananchi kujitokeza katika eneo hilo ili kuweza kupata huduma hizo za afya bure. 

Alisema huduma wanazotoa bure siku nzima ya leo ni pamoja saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti, elimu kuhusu lishe bora, shinikizo la damu (BP), sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji watoto kwa akinamama. 

 "Kuelekea maadhimisho ya siku yetu, tumejitolea kupima afya bure kwa wananchi wote watakaojitokeza katika eneo hili...huduma zinazotolewa bure leo ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti, tunatoa elimu kuhusu lishe bora, tunapima shinikizo la damu (BP), tunapima sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji," alisema Bi. Elizabeth Thawe. 

 Aliongeza kuwa huduma hizo zinatolewa kwa wanachama wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) tawi la Muhimbili kwa kushirikiana na wengine kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na vyuo vyote vya afya vinavyozunguka Hospitali ya Muhimbili.

 Alisema mbali na kutoa huduma hizo bure siku ya pili ya maadhimisho (yaani Agosti 7, 2017) watafanya kongamano la kisayansi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku hiyo muhimu kwa wakunga. Aidha aliishukuru Benki ya NMB ambayo ni wadhamini wa kuu wa maadhimisho hayo pamoja na makampuni mengine yaliojitokeza kusaidia kufanikisha shughuli hizo. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia misululu ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure eneo hilo na wengine kuvutiwa na huduma za NMB zilizotolewa eneo hilo, kuwaunganisha wananchi na huduma za kibenki.  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa