Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » STARTIMES NA SIBUKA KUDHAMINI LIGI YA KIKAPU.

STARTIMES NA SIBUKA KUDHAMINI LIGI YA KIKAPU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Agness Moshi
Kampuni ya kurusha matangazo kwa njia ya digitali na waauzaji wa ving’amuzi Startimes na Shirika la utangazaji la Sibuka waidhamini ligi ya mpira wa kikapu Dar es Salaam (RBA).
Hayo yamesemwa na Afisa Mahusiano wa Startimes Bw. Samuel Gisayi wakati akitambulishwa na Chama Cha Mpira wa Kikapu (BD) kwa waandishi wa habari kuwa mdhamini mpya wa RBA, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Gisayi amesema kuwa udhamini kwa ligi hiyo kwa sasa ni wa muda mfupi, na baada ya kumalizika kwa ligi ya RBA wako kwenye mazungumzo ya kuwa wadhamini wa mojakwa moja wa mchezo huo kwa kipindi cha miaka mitano.
“Tumeamua kudhamini RBA ili kukuza vipaji vya wacheza mpira wa kikapu kwa sababu Makampuni mengi yamekua yakiwekeza kwenye mpira wa miguu na kusahau mchezo huu kusaidia wachezaji waweze kuonekana na kusajiliwa kwenye timu kubwa” , alisema Bw.Gisayi.
Bw.Gisayi ameongeza kuwa tayari wamefanya mambo mbalimbali ili kuweza kufanikisha mashindano hayo ikiwemo kuboresha viwanja ambavyo mchezo huo utafanyika na kudhamini gharama zote za uendeshaji wa ligi hiyo kuanzia mzunguko wapili mpaka fainali.
“Ukiachana na uuzaji wa ving’amuzi Startimes inashirikiana na Jamii katika kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo ili kuinua vipaji vya Watanzania” ,alisititiza Bw.Gisayi.
Bw.Gisayi ametoa wito kwa wafanyabiashara kupeleka matangazo yao kwenye vituo vyao ili waweze kutangaziwa kwa bei rahisi wakati wa ligi hiyo , pia ametaka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa mchezo wa mpira wa kikapu kama michezo mingine .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa habari na Mawasiliano Bw.Peter Mpangala amesema kuwa wanaimani mchezo huo utafika mbali na utakua wa kibiashara kupitia udhamini wa startimes na sibuka kwasababu wamepata kupata fursa ya kuwa na kurusha michezo yao mubashara kwenye televisheni.
“Ukiwa na kipindi kwenye televisheni unakaribisha wadau wengi zaidi kuudhamini mchezo na tunategemea biashara kubwa kwa wachezaji”, alisema Bw.Mpangala.
Bw.Mpangala ameongeza kuwa amefurahishwa na kitendo cha startimes kuwadhamini kwa sababu kupitia kampuni hiyo ambayo inashirikiana na taasisi ya kubwa inayosimamia mchezo huo Duniani (FIBA) wataweza kufikia malengo ya kuufikisha mchezo huo mbali.
Naye ,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Okare Emesu amesema kuwa, wana mikakati ya pamoja na wadhamini hao ili kuufanya mchezo huo uwe wa kibiashara na uweze kufika mbele zaidi, vilevile ametoa wito kwa wananchi kufuatilia vipindi vya mchezo huo vitavyoonyeshwa kwenye king’amuzi cha startimes kupitia Tv Sibuka kila siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili saa kumi na mbili jioni.
Ligi ya RBA kwa sasa ipo kwenye mzunguko wa pili na baada ya wiki 3 hatua ya mtoano (playoff) itaanza rasmi kuelekea fainali itakayofanyika tarehe 24 mwezi huu Uwanja wa Taifa .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa