Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MTANDAO WA TGNP WAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

MTANDAO WA TGNP WAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM





Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokutanishwa ili kujadili namna ya kufanya kazi katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.


Balozi Getrude Mongella akizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari leo kuhusu maandalizi ya Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.


Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akizungumza jambo wakati wa semina iliyowakutanisha waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali iliondaliwa na Mtandao TGNP .



Baadhi ya wahariri pamoja na wafanyakazi wa Mtandao TGNP wakiwa kwenye semina


Afisa Habari wa TGNP ,Monica John akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliofika kwenye semina iliyokuwa inahusu tamasha la wanawake litakalofanyika jijini Dar mwaka huu.




Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakichangia mada kwenye semina iliyowakutanisha ili kujadili namna nzuri ya kufanya kazi katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.


Picha ya Pamoja

TGNP Mtandao kutambua mchongo wa wanawake walioshiriki kuleta maendelea nchini hapa nchini Tanzania katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na katika semina ya kutoa elimu juu ya tamasha hilo kwa Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Lihundi, alisema lengo la tamasha hilo ni kusherehekea, kujadili changamoto na mafanikio ya harakati wanazozifanya.

Alisema Tamasha hilo litawahusisha wanawake mbalimbali ambao wamepata mafanikio makubwa katika harataki za ukombozi wa mwanamke na kuhakikisha usawa wa kijinsia.

“Katika siku zote nne wanawake zaidi ya 1000 watakaa na kujadili changamoto zinazoikumba jamii, kusherekea mafanikio yaliyopatikana  na kujenga nguvu ya pamoja katika kuhakikisha ukatili wa kijinsia unaisha.

“Kutokana na kauli mbiu ya tamasha hili inavyosema kuwa Mageuzi ya Mfumo Kandamizi kwa Usawa wa Kijinsia na Maendeleo. Tunakata kuangalia mwanamke anaonekana vipi katika hazma ya Serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda,” alisema Lilian.

Aidha alisema wajasilimali wataonesha bidhaa na kupata elimu ya namna gani wanaweza kuboresha bidhaa zao na ufungashaji ili waweze kuingia kwenye soko la ushindani la bidhaa za ndani na nje ya nchi kutoka Shirika la Viwanda vidogo (Sido), Mamlaka ya Chakula a Dawa (TFDA) na Taasisi ya Udhibiti Ubora (TBS) kwa ajili ya kupewa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa