Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Utawala na Maendeleo ya Uwezeshaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
. Profesa wa Menejimenti ya Elimu kutoka Skuli ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Eustella Bhalalusesa (katikati) akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha muwasilisha mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo, Peter Lanya akizungumza machache kabla ya kumkaribisha muwasilishaji mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka ESRF, John Shilinde akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Hildegalda Mushi kutoka COSTECH akichangia maoni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mshiriki William Mhoja akichangia mada kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof Honest Prosper Ngowi akishiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption]
Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
PAMOJA na serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, ikiwa ni
asilimia 17 ya bajeti nzima, mazingira ya kufundisha na kufundishwa
nchini bado si mazuri.
Akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni
kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya
serikali 2017/18 katika elimu na kilimo Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli
ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na kuwekwa maeneo ya
kuangaliwa kwanza ipo haja ya kufanya zaidi ili kufikia malengo.
Dk Katabaro katika mada yake alisema kwamba pamoja na serikali kutenga
zaidi ya TZS 1.366,685,241,000.00 katika Wizara ya Elimu, Sayansi na
Ufundi huku Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali ya Mitaa
(TAMISEMI) ikipatiwa sh 201,655,446,000/- kwa ajili ya elimu, alisema
kwamba anaona ipo haja ya kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa ili
kuweka sawa mazingira ya kufundisha na kufundishwa.
Katika
mjadala huo wa kitaifa uliodhaminiwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi
na Kijamii (ESRF), Dk Katabaro alisema kwamba kwa sasa vifaa vya
kufundishia na kujifunzia vinakosekana katika shule nyingi na taasisi
zinazohusiana na elimu na hivyo kukwamisha ufanisi na tija katika elimu.
Aidha
katika mada yake alitaka juhudi inayofanywa ya kuweka sawa mizania ya
walimu pale walipo wengi kuhamishwa inabidi iendelee ili kuweka uwiano
sawa wa elimu nchini.
Pia
alisema kuwa uwiano wa sasa wa walimu nchini sio sawa huku katika
masomo, baadhi yakiwa na walimu wa ziada na mengine yakiwa na upungufu
mkubwa
Mwaka
2016 kwa mujibu wake kulikuwa na walimu wa ziada katika masomo kadha
huku kukiwa na upungufu katika masomo mengine hasa Hesabu na Sayansi:
Basic Mathematics – 7,291 (Upungufu);Biolojia – 5181 (Upungufu);Kemia –
5373 (Upungufu);Fizikia – 6873 (Upungufu);Kilimo 508
(Upungufu);Kingereza– 1267 (ziada); Jiografia – 3281 (ziada); Historia –
4764 (ziada) na Kiswahili – 4795 (ziada).
Pamoja
na masomo Dk. Katabaro aliangalia bajeti hiyo katika maeneo muhimu
yanayofanya mtoto kuwa na akili kama viwanja vya michezo na upatikanaji
wa maji safi kwa ajili ya kunywa na usafi.
Maji haya ni muhimu sana kwa watoto wa kike ambao usafi wao ndio siri ya mahudhurio ya shule kila siku.
Mada
hiyo pia ilitahadharisha kuhusu takwimu ikitaka zitumike vyema ili
kuondoa mipango mibovu hasa ya uandikishaji wa watoto wa darasa la
kwanza na wale wanaoingia kidato cha kwanza.
Wakati
huo huo katika mada iliyowakilishwa kwa pamoja kati ya Profesa haidari
Amani na John Shilinde, kilimo pamoja na kutegemewa na wengi na kuwa
chachu ya maendeleo ya viwanda bajeti yake iliyotengwa bado ni ndogo
Walisema
kwamba sekta hiyo ilipata kiasi cha karibu asilimia 10 ya bajeti nzima,
bajeti ambayo ukiiangalia utaona kwamba haiwezi kubadili kilimo.
Wamesema kwamba kilimo ambacho huajiri asilimia 70 ya wananchi
ikichangia asilimia 28 ya pato la taifa huku ikipatia asilimia 30 ya
mapato ya kigeni na kuchangia asilimia 65 ya mali ghafi, bado sekta
haijapewa nguvu za kutosha kusonga mbele.
Wamesema kilimo
kitabadilika kwa fedha za utafiti na sayansi na ubunifu ili kuiweka
sekta katika hali bora zaidi.
Walisema kwamba sayansi na ubunifu ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko
katika kilimo.
Wataalamu hao walitaka bajeti zaidi kwa ajili ya utafiti na maendeleo,
kilimo cha umwagiliaji, kuongeza ruzuku, kuboresha kilimo cha kisasa cha
kutumia zana kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza kazi
zenye staha vijijijni, kuongeza mnyororo wa thamani na matumizi endelevu
ya ardhi na maji.
0 comments:
Post a Comment