Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WENYE MASHAMBA WALIYOKOPEA KITANZINI

WENYE MASHAMBA WALIYOKOPEA KITANZINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Imeandikwa na Halima Mlacha
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Moses Kusiluka
KATIKA jitihada za kuwadhibiti wafanyabiashara wa mashamba makubwa wanaoyatumia kwa ajili ya kukopea fedha na kisha kutoyaendeleza, serikali inatarajia kuanzia mwakani, kuwasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ardhi, utakaowadhibiti wafanyabiashara hao.
Hatua hiyo, imetokana na namna Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilivyobaini uwepo wa mashamba mengi yakiwemo yanayomilikiwa na wafanyabiashara wakubwa nchini ambayo hayajaendelezwa huku yakiwa yamekopewa fedha nyingi na kutumika katika biashara nyingine.
Akizungumza na magazeti ya Serikali ya HabariLeo na Daily News ofisini kwake Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Moses Kusiluka alisema sheria hiyo italenga kudhibiti watu kutumia mashamba kujipatia fedha na kisha kuyatelekeza.
“Tunataka kupitia sheria hii, mtu akikopa kupitia mashamba haya, fedha hizo zitumike kuyaendeleza na siyo kuyaacha mapori na kufanya biashara zake nyingine. Sheria itaweka masharti kuwa mikopo yote yenye dhamana ya mashamba, isimamiwe na benki zenyewe,” alisema.
Alisema katika mpango unaoendelea wa kushirikiana na halmashauri za wilaya kufanya ukaguzi wa mashamba yasiyoen-delezwa wamebaini mashamba mengi ambayo hayajaendelezwa yakiwemo yaliyochukulia mikopo benki. “Mashamba yote yasiyoendelezwa baada ya kufuata taratibu zote, ikiwemo kutoa notisi kwa wamiliki tumeyawasilisha kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya kubadilishiwa umiliki.
Haya yaliyochukulia mikopo, sheria inaturuhusu kuyataifisha pia,” alisema. Hata hivyo, alisema mashamba hayo yaliyochukulia mikopo kwa sasa wanazungumza na benki husika ili kuangalia namna ya wahusika wa mashamba hayo kubadili dhamana za mikopo yao ili yaweze kurejeshwa mikononi mwa serikali.
“Tunafanya hivi si kwa sababu eti hatuna uwezo wa kuyachukua la hasha, tunafanya hivi ili kunusuru benki hizi, kwani mashamba mengi yamechukulia mikopo mikubwa endapo tutayataifisha na kuyachukua kama hakuna dhamana nyingin
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa