Tuesday, April 3, 2012

RIPOTI YA WATALII WALIONDOKA NCHINI MWAKA 2010 YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao akizindua kitabu cha ripoti ya watalii walioondoka nchini mwaka 2010 ambapo ametoa wito kwa wadau wote wa utalii watumie matokeo ya ripoti hiyo kuboresha shughuli na huduma zao katika kutangaza utalii na kuandaa mazao (products) ili kuwavutia watalii wengi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili Bw. Ibrahim Mussa.
Na.MoBlog Team
Ripoti hii ya watalii wanaonondoka nchini huandaliwa  kila mwaka ili kujua hali halisi ya sekta ya utalii kwa mwaka husika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao amesema sekta ya Utalii imekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza pato la taifa na pia fedha za kigeni nchini.
Amesema ripoti hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya sekta ya Utalii kwani pamoja na kutupatia taarifa mbalimbali za Utalii lakini pia inatoa taarifa ya changamoto ambazo tunazo katika sekta hii na hivyo kuweza kuzifanyia kazi kwa muda muafaka.
Pamoja na mambo mengine taarifa inayotolewa inasaidia kujua mambo yafuatayo :
·         Wastani wa fedha anazotumia mtalii kwa siku
·         Wastani siku ambazo mtalii kwa kwa wakati wote anapokuwa nchini
·         Masoko /nchi zinazoleta wageni wengi nchini
·         Mapato ya jumla yanayotokana na bishara ya Utalii kwa mwaka husika.
Nakala za ripoti hii zitapatikana hapa wizarani, Benki Kuu, Ofisi ya taifa ya Takwimu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa hisani ya Mo Blog

No comments:

Post a Comment