Waziri wa Nishati na Madini Mh. Willian Ngeleja akitoa maelezo kuhusu maonesho ya kimataifa ya vito ya Arusha kwa mwaka 2012 ambapo amesema maonesho hayo yatawakutanisha wafanyabiashara wa madini ya vito kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, pamoja na wataalam wa kimataifa wa madini ya vito, wawakilishi wa serikali na wadau wengine wa tasnia ya vito. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini Ally Samaje.
Kaimu Kamishna wa Madini Ally Samaje akijibu maswali ya waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwa kuwa kupitia maonesho hayo ya kikanda, nchi husika zitaweza kuonesha rasilimali zilizopo na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuendeleza shughuli za uongezaji thamani katika madini ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi husika kwa namna endelevu zaidi. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. Willian Ngeleja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Adam Malima.
No comments:
Post a Comment