Zaidi ya wasimamizi 400 wa zoezi la sensa katika kituo cha Mtakuja Kata ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni asubuhi hii wamekusanyika katika shule ya Mtakuja wakishinikiza kulipwa malipo yao kwa kushiriki katika mafunzo ya sensa yaliyofanyika kwa siku tisa.
Habari zilizotufikia kutoka kwa baadhi ya washiriki hao zenasema kuwa wamelazimika kufanya mgomo huo kufuatia waratibu wa sensa kata hiyo kutangaza kuwalipa sh, 175,000 badala ya sh.300, 000 kwa madai kuwa serikali haina pesa ya kuwalipa pesa zao kwa mkupuo.
Wasiamizi hao wamesema kuwa wanakamilisha makubaliano miongoni mwao ili kugoma na kuandamana hadi katika ofisi za Wilaya kudai malipo yao kwa kuwa katika wilaya nyingine wasimamizi wamelipwa pesa zao zote.
Habari ambazo hazijadhibitishwa zinasema kuwa waratibu hao wa zoezi wanahofia kutoa malipo yote kwa wasimamizi hao kwa madai kuwa wanaweza wasirudi katika zoezi lenyewe na kutokomea na pesa hizo.
Jitihada za kupata mratibu wa sensa kata ya Kunduchi zinafanyika na punde tukizipata tutakujuza
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment