KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM
(UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba
(UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba
Neema akikabidhiwa fomu jana na Sophia Duma Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam .
--
DAR ES SALAAM, TANZANIA
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM
(UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba, amejitosa kwenye
uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na
uwakilishi UWT.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana, Agosti 3, jijini Dar es
Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya
Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,
Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini
Uingereza, alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni
kuakikisha mikakati thabiti inajengeka kwa kiwango kikubwa miongoni
mwa vjana na wanawake wote nchini.
“Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu
ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia
wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa
na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.
Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari
alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.
Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua
fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.
No comments:
Post a Comment