na Agness Newa na Stella Mushi
ADIA Michael (20), mkazi wa Yombo Sigara jijini Dar es Salaam, anashikiliwa na polisi baada ya kumtupa chooni mtoto wake wa kiume mwenye umri wa siku nne.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa kichanga hicho kiliokolewa juzi na majirani baada ya kusikia sauti yake ikitokea chooni.
Alisema majirani hao walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo akiwa hai baada ya kuvunja upande mmoja wa choo hicho.
Kwa mujibu wa Misime, mama huyo alipohojiwa alikiri kukitupa kichanga hicho kwa madai kuwa maisha ni magumu.
Alisema kichanga hicho kimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, huku mama yake akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment