Kada wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Daud Msungu
(kushoto), akirejesha fomu za kuomba kugombea nafasi ya makamu
mwenyekiti wa umoja huo, kwa Sophia Duma ambaye ni Mkuu wa Idara ya
Organaizesheni Makao Makuu ya UVCCM, Dar es Salaam jana. Msungu
alikuwa mjumbe wa Baraza la umoja huo kupitia Mkoa wa Lindi.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kurejesha fomu hizo,
Msungu, alisema endapo akifanikiwa kugombea na kushinda wadhifa huo,
atamshauri mwenyekiti, kuweka mikakati ya kuwashawishi vijana kushiriki
katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya Taifa, kwa vile
vijana ndiyo nguvu ya Taifa.
Pia amesema kuwa, atahakikisha wanarudisha umoja na mshikamano kwa vijana kwa ajili ya ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.
"Hiyo
itasaidia vijana kusukuma mbele, gurudumu la maendeleo ya Taifa letu,
kuendana na kasi ya kiuchumi na maendeleo hasa katika kipindi hiki cha
mabadiliko ya kiuchumi yanayoendelea duniani" alisema Msungu.
Atashirikiana
na viongozi wengine wa umoja huo, kuandaa mipango ya mafunzo kwa
vijana kuielewa vizuri itikadi ya chama, hasa kwa kufufua vyuo
mbalimbali vya itikadi ikiwemo Kambi ya Ihemi, mkoani Iringa..

No comments:
Post a Comment